Na Karoli
Vinsent
KUFUATIA mchezaji Emmanuel Okwi kuikacha
klabu ya Yanga na kujiunga kwa wapinzania wa Jadi wa timu hiyo, Klabu ya
Simba.
Mwenyekiti wa Klabu Yanga Yusuph Manji ameibuka na kuwataka wanachama
pamoja na Mashabiki wa Yanga kuwa wapole katika kipindi hiki,na Badala yake
Yanga wamesema wanataka Fidia kutoka kwa Mchezaji huyo pesa za kimarekani dola
laki tano, sawa na pesa za Kitanzania zaidi ya milioni 700 kwa kitendo chake
cha kuvunja sheria za mpira wa miguu nchini.
Hayo yamesemwa mda huu Jijini
Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Yanga,Yusuph Manji wakati wa Mkutano na
Waandishi wa Habari kuzungumzia suala
nzima la usajili,ambapo Manji amesema klabu hiyo haina ugomvi na Simba kwani
wameshirikiana sana kwenye mambo mengi ila
anashangaa rafu mbaya iliyofanyiwa klabu hiyo,wakati wa kumsajili
Emmanuel Okwi.
“Kiukweli Klabu ya Simba ni marafiki
zetu sana ila nashangaa jinsi
walivyotufanyia kwenye usajili wa mchezaji Emmanuel Okwi maana ni
rafu,kwasababu ukisoma sheria ya mpira wa miguu ya FIFA namba 17 kigungu cha
tano kinasema wazi kuhusu usajili ni kwamba klabu yeyote inaotaka kumsajili mchezaji
wa timu nyingine inapaswa kuwasiliana na Timu husika,lakini wenzetu Simba hawajawasiliana
na sisi,kutokana na hujuma hii yanga tunataka fidia za dola laki tano sawa na
pesa za Kitanzania zaidi ya milioni 700 ”alisema Manji.
Manji
alizidi kusema Klabu ya Yanga tayari imeliandikia barua shirikisho la Soka
nchini TFF na kuwapa siku saba wawe wametoa hukumu kwa Simba ikiwemo kulipwa fidia
hiyo,
Aidha Manji
alisema Klabu hiyo haisikitiki kwa kuondoka kwa mchezaji huyo kwani wachezaji
wengi waliokuwapo Klabuni hapo na wameondoka ila wao wanasikitika kwa kuvunjwa
Sheria .
“Mimi
nashangaa sana watu wanavyosema Yanga inametuhuma sana kuondoka kwa Okwi,ila
jibu ni hapana kwani hapa Yanga wameondoka wakina Kavumbagu,Domayo wamekwenda
klabu ya Azam mbona hatujasikitika?kwanza Okwi ni mchezaji wa Kawaida sana naweza
kusema katika mechi 13 za ligi
alizocheza Yanga msimu uliopita katika mechi sita kashinda goli moja tu sasa
tumsikitike nin?”alisema Manji.
Vilevile mwenyekiti huyo aliwataka Wanachama
pamoja na wapenzi wa Yanga nchini kuwa wapole na kuuwaachia uongozi wa Yanga
unavyolishughulikia suala hilo.
Habari za Mchezaji huyo wa Kimataifa kutoka Uganda Emmanuel Okwi kuihama klabu hiyo zilizopatikana jana jioni, zilisema nyota huyo ambaye hatima yake ndani ya klabu ya Yanga ilikuwa gumzo kubwa, jana alitarajiwa kusaini mkakaba huo kuwatumikia Wekundu wa Msimbazi kwa kipindi kingine.
Kurejea kwa Okwi Msimbazi, kunamweka katika wakati mgumu mchezaji Benard Musoti, nyota wa kimataifa wa Kenya, kwani sasa ni yeye anayechungulia dirisha la kutokea, ama Pierre Kwizera.
Okwi kutua Simba, ni kama kurejea nyumbani kwani ndio klabu aliyojiunga nayo kwa mara ya kwanza nchini akitokea Uganda na kung’ara nayo, kabla ya kuihama na kujiunga Etoile du Sahel ya Tunisia na kisha Yanga.
Sheria za usajili za Ligi Kuu Tanzania Bara zinataka klabu kuwa na nyota wa kigeni wasiozidi watano na mbali ya Okwi, nyota wengine wa kimataifa katika kikosi cha Simba ni, Raphael Kiongera, Joseph Owino, Musoti, Kwizera na Amisi Tambwe.
Mapema jana kabla ya Okwi kutua Simba, benchi la timu ya Simba, lilisema bado linamuhitaji Donald Musoti na kudokeza kuwa, haliridhishwi na kiwango cha Hussein Butoyi.
Butoyi, nyota wa kimataifa wa Burundi aliyetua Simba, hivi karibuni kuziba nafasi ya Musoti aliyekuwa mbioni kutemwa, lakini akishindikana kutokana na ugumu wa mkataba wa nyota huyo.
Musoti, ambaye miongoni mwa nyota Simba waliofanya vema msimu uliopita, amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
Habari zilizopatikana jana kuutoka ndani ya Simba, zilisema, baadhi ya viongozi walimuhitaji Butoyi na wengine wakisapoti hatua ya benchi la ufundi kumtaka Musoti kutokana na kiwango chake.
“Benchi la ufundi, linamuhitaji Musoti aendelee kukipiga Simba, hata mimi binafsi, Musoti namuona anafaa, huyo Butoyi hamna kitu kabisa, wanaosema wanalingana uwezo sio kweli, Musoti anajua bwana,” kilisema chanzo hicho.
No comments:
Post a Comment