Mwenyekiti wa baraza la vijana BAVICHA bw PATROBAS KATAMBI akizungumza na wanahabari muda huu hapa katika mkutano wa chadema unaoendelea |
Kufwatia jeshi la polisi Tanzania jana kupiga
marufuku maandamano yaliyotangazwa kufanyika na chama cha democrasia na maendeleo
CHADEMA,umoja wa vijana wa chama hicho BAVICHA umeibuka na kusema kamwe
hawatishiki na kauli ya jeshi hilo na wapo tayari kwa lolote.
Akizungumza
na wanahabari muda huu nje ya mkutano wa kamati kuu ya chama hicho mwenyekiti
wa vijana taifa PATROBAS KATAMBI amesema kuwa kauli iliyotolewa na mwenyekiti
wao sio kauli yake kwani ni kauli ya chama na wanachama wote hivyo polisi
wasihangaike kumkamata mwenyekiti wao na badala yake wajiandae kulinda amani
wakati wa maandamano hayo.
“tumezoea
kusikia kauli za vitisho vya jeshi la polisi wakati chadema inapotaka kufanya
kitu cha kuwatetea wananchi wao,ila siku ccm ikitangaza kufanya maandamano ya
amani huwezi kusikia kauli kama hizo,sasa tumechoka na mambo hayo na tupo
tayari kwa lolote lile”amesema mwenyekiti wa BAVICHA TAIFA
Aidha amesema
kuwa ofisi yake imeitisha kikao cha dharura kwa ajili ya kupanga mikakati imara
ya kuanza maandamano hayo ambapo amesema kuwa yatafanyika nchi nzima bila
kikomohuku akisema yataanza muda wowote
kuanzia sasa.
Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama hicho WILFRED LWAKATARE akizungumza na wanahabari muda huu |
Katika hatua nyingine mkurugenzi wa ulinzi na
usalama wa chama hicho WILFRED LWAKATARE amesema kuwa wao kama watu wa ulinzi wa chama
hicho wanatekeleza lile ambalo limetotangazwa na viongozi wao wa juu hivyo ni
jukumu lao kuhakikisha kuwa maandamano hayo yanafanyika kwa amani na kama
itatokea vurugu itakuwa imeletwa na polisi wenyewe.
No comments:
Post a Comment