Tigo
Tanzania leo imetangaza udhamini wake kwa maonesho ya filamu barani Afrika yatakayofanyika
mkoani Arusha kuanzia Jumamosi wiki hii. Maonesho hayo ya wiki moja yanayojulikana
kama maonesho ya filamu za Kiafrika Arusha (AAFF) yataonesha filamu mbali mbali
za wasanii nchini na kimataifa.
Akitangaza
udhamini huo kwa waandishi wa habari kutoka ofisi za Tigo Arusha, Mkurugenzi wa
Kanda ya Kaskazini wa Tigo, David Charles alisema kwamba udhamini huo wa Tigo
katika maonesho hayo ya filamu ni dhamira ya dhati ya kampuni hiyo katika
kuendeleza tasnia ya filamu nchini ambayo kwa sasa inatoa ajira kwa maelfu na
maelfu wa vijana nchini na kuwainua kimaisha.
“Tasnia
ya filamu nchini imebadilika kutoka kuwa tasnia ambayo inaburudisha wapenzi
wake na kuwa sekta inayotoa ajira kwa vijana. Tunaamini kwamba AAFF ni fursa
nzuri kwa waigizaji na waandaji wa filamu kuonyesha vipaji vyao na kutangaza
pia utamaduni wa Tanzania kimataifa,”alisema Charles.
Meneja wa Mawasiliano wa Tigo Bw. John Wanyancha(aliyesimama) akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha leo wakati wa mkutano kuhusu udhamini wa Tigo maonesho ya AAFF. |
Ukitoa kutazama filamu, kutakuwa pia na
warsha na semina ambazo zitaongelea mada mbali mbali kuhusu maendeleo ya tasnia
ya utengenezaji filamu barani Afrika kama ushirikishwaji wa vijana, mshikamano
wa kijamii na kiutamaduni, na jinsi ambavyo hayo yanahusiana na maendeleo ya
kiuchumi na kijamii katika jamii zetu. Warsha na semina hizo zitawahusisha
washiriki kutoka nchini Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi, nchi zote
za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), alisema Birdi.
Mkurugenzi wa maonesho ya AAFF Akpor
Otebele, “Napenda kuwaalika wapenzi wote wa filamu kutoka Tanzania na nchi
jirani za Afrika Mashariki kuweza kuungana nasi katika maonesho haya ya AAFF
kuanzia Jumamosi tarehe 20 mpaka Jumamosi tarehe 27 Septemba waweze kushuhudia vipaji
vya wasanii nchini na wa kimataifa na kusikia simulizi nzuri kutoka barani
Afrika.”
No comments:
Post a Comment