KUFUATIA taarifa mbalimbali zilizokuwa zimezushwa na kusambazwa kwenye simu pamoja na Mitandao ya kijamii kwamba Mwandishi Mwandamizi na Mzalendo wa Nchi yake, Saed Kubenea amepigwa Risasi na hali yake kuwa mbaya,sasa hivi ndivyo mwenyewe alivyojibu
"Taarifa zimetupwa kwenye mitandao ya simu, zikisema kuwa mimi Saed Kubenea, nimejeruhiwa kwa risasi na kwamba hali yangu ni mbaya sana. Imeelezwa kuwa tukio hilo lilitokea leo majira ya saa tano asubuhi katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Binafsi nimejulishwa tukio hilo na Mwandishi wa habari wa Star TV na baadaye nikaelezwa kuwapo uvumivu huo na Katibu wa Jukwaa la Wahariri, Neville Meena.
Napenda kuujulisha umma kuwa habari hizo siyo kweli. Mimi niko salama na naendelea na majukumu yangu kama kawaida”alisema Kubenea
Ikumbukwe Kubenea ni Mwandishi wa Gazeti la Mawio na mmiliki , MwanaHALISI Online.com na mtandao wa MwanaHALISI Forum pamojaMkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited - wachapishaji wa gazeti la MwanaHALISI, lilosimamishwa na serikali kwa muda usiojulikana, MSETO,ambapo kubenea ambaye amefungua kesi Mahakama kuu kushinikiza Bunge Maalum la Katiba livunjwe kutokana na bunge hilo kupoteza pesa za Watanzania
No comments:
Post a Comment