Wednesday, September 3, 2014

Microsoft Windows Phone 8.1yatambulishwa Tanzania kupitia Lumia 930, Lumia 630 and Lumia 530

Meneja mawasiliano wa microsoft mobile divice akizungumzia uzinduzi huo
 KAMPUNI ya Microsoft leo imetambulisha aina tatu ya Lumia ambazo ni Lumia 530, Lumia 630 pamoja  na Lumia 930 huku zikiwa zimeunganishwa kabisa na mfumo mpya na wa kisasa wa kiteknolojia wa uendeshaji wa simu wa Windows Phone 8.1.

Mfumo huo mpya wa Windows Phone 8.1 unatoa mwanya zaidi kwa watumaiji wa simu hizo kuhakikisha kuwa wanajiunganisha na huduma mbalimbali za kisasa hasa katika lumia 530.

Pia kupitia mfumo huo wataalamu wa masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wanakuwa na mwanya mpana zaidi wa kuweza kujitengenezea bidhaa mbalimbali za kiteknolojia kupitia hiyo Window Phone 8.1.
Meneja wa bidhaa wa Microsoft, Kingori Gitahi akizungumza wakati wa kutambulisha huduma hiyo mapema leo jijini Dar es salaam
 Meneja wa bidhaa wa Microsoft, Kingori Gitahi alisema kuwa  kupitia bidhaa hizo mtumiaji anakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi kutumia huduma kama vile za mawasiliano ya moja kwa moja kwa njia ya Skype na zile za Microsoft Office.

      Alisema kuwa watumiajiwasimuhizowanakuwanawakatimzurizaidikatikakujipatia huduma za uhakika za mitandao ya kijamii kama vile Instagram, WhatsApp, Viber na WeChat.

      Aliongeza kuwa inamfumomzurizaidiwamatumiziyaKamera kwa kiwango kikubwa cha 5MP huku ikiwa ni rahisi kuunganishwa kwa matumizi ya huduma za laini mbili za simu.
       
      "Pia ina kadi yenye ukubwa wa 4GB ambayo inayoweza kuunganishwa na kuongeza uwezo wake wa kazi kupitia kadi ya hadi kiwango cha 128GB," alisema Kingori.
      Aliongeza kuwa " pia kwa kupitia mfumo huo wa Microsoft pia mtumiaji anajipatia zaidi kiwango cha15GB ambapo mtumiaji huyo atakuwa kwenye wakati mzuri wa kutumia huduma hizo akiunganishwa na computers, laptops na tablets".
 Aliongeza kuwa kupitia bidhaa ya Lumia 630 mteja anakuwa na uwezo wa kupata huduma za Nokia Mapambazo inamwezesha wapi anaelekea na wapi anatokea.

Alisema kuwa hali hiyo inasaidia kwa kiasi kikubwa mteja kufurahia huduma mbalimbali za Nokia Map huku akiwa na wakati mzuri wa kuweza kubabilisha rangi ya muonekano wa simu yake.

Alifafanua kuwa katika simu za Nokia 930 kuna huduma mbalimbali ikiwamo inayomwezesha mteja kujua ni kiwango cha matembezi aliyotembea, amepungua kilo ngapi ikiwa pamoja na kumwelezea umbali wa kiwango alichotembea.

Alisema kuwa ina kiwango kikubwa cha kurekodia Video huku ikiwa na uwezo mkubwa wa kuchuja sauti na kurekodi vizuri zaidi.

 Alisema ina wireless charge uwezo mkubwa wa picha kwa umakini kama camera ya kawaida ikiwa na kiwango cha 1080p Full HD huku ikiwa na betrii yeye uwezo mkubwa wa kuhifadhi umeme  kwa kiwango cha hali ya juu.

Aliongeza kuwa aina hizo zote za Nokia Lumia zina huduma ya bure ya hera Map ambapo mtumiaji anaweza kujua ni wapi alipo wapi aendako pia.

Alisema kuwa ni fursa nzuri kwa mtumiaji hasa mtalii kujua huduma aitakayo katika mahala alipo, huduma kama vile migahawa, benki na nyinginezo ambapo kupitia huduma ta Here Map mtumiaji anaweza kupata hadi namba za simu za watoa huduma husika inayotafutwa.

Alisema kuwa kwa sasa bidhaa hizo zinapatikana kwa bei tofauti ambapo lumia 530 ni Shilingi 240,000, Lumia 630  inauzwa shilingi 345,000 huku Lumia 930 ni shilingi 1,200,000.

No comments: