Wafanya biashara wa maduka katika soko la kariakoo jijini Dar es salaam leo wameamua kufunga maduka yao ikiwa ni sehemu ya kile ambacho kinatajwa kuwa ni mgomo wao wa kimya kimya ambao umeanza leo. Mwandishi wa mtandao huu hadi sasa ameweka kambi katika soko hilo na hadi sasa sehemu kubwa ya soko hili maduka yake yamefungwa na huku wafanya biashara hao wakiwa hawapo kabisa katika maduka hayo. Chanzo cha mgomo huu bado hakijawekwa wazi na wahusika hao ila habari zinasema kuwa ni mwendelezo wa migomo yao ya kupinga matumizi ya mashine za kielectronic za EFD. HABARI ZAIDI ZITAKUJIA HAPA |
No comments:
Post a Comment