Wednesday, September 24, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA MWAKA LA WAKAGUZI WA HESABU ZA NDANI JIJINI ARUSHA LEO.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua Kongamano la mwaka la siku tatu la Wakaguzi wa Hesabu za Ndani, linaloendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha. Kongamano hilo limefunguliwa leo Septemba 24, 2014. Picha na OMR

 Baadhi ya washiriki waliohudhuria Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia katika ukumbi wa AICC jijini Arusha leo Septemba 24, 2014.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia burudani ya ngoma ya asili wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa AICC jijini Arusha leo Septemba 24, 2014 kwa ajili ya kufungua Kongamano la mwaka la siku tatu la Wakaguzi wa Hesabu za Ndani. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, amkabidhi zawadi Shadrack Kishimba, kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la mwaka la siku tatu la Wakaguzi wa Hesabu za Ndani, linaloendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha. Picha na OMR

Picha ya pamoja na washiriki wa kongamano hilo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Dkt. Joan Pastor, (kulia) na Lesedi Lesetedi baada ya kufungua rasmi Kongamano la mwaka la siku tatu la Wakaguzi wa Hesabu za Ndani, linaloendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha. 



No comments: