Na karoli Vinsent
SERIKALI ya Tanzania imezidi kuuzika uhuru wa Habari nchini kutokana na sasa kuanza kuvifungia vyombo vya Habari hususani Magazeti,baada ya hivi sasa serikali kujiweka tayari kuyafungia magazeti ya Nipashe,Tanzania Daima pamoja Mawio,Mtandao huu unaripoti
Taarifa za kuaminika ambazo mtandao huu umezipata zinasema serikali imejipanga kuyafungia magazeti hayo kutokana na habari wanazoziandika ambazo serikali inaziita ni za uchochezi,
Kwa mujibu wa Vyanzo mbalimbali zinasema serikali imekasirishwa na Habari wanazoziandika magazeti hayo kuhusu mwenendo wa Bunge Maalum la Katiba ambazo wanadai habari hizo zinaleta mgongano kwa wananchi,
Mpashaji huyo wa Habari aliuambia mtandao huu kwamba kwasasa serikali imejipanga kuhakisha inayafungia magazeti hayo.
“Sikiliza sahivi serikali imechoka sana na mwenendo wa haya magazeti nchini,yaani yamekuwa yakiaandika habari ambazo ukizisoma utazijua tu ni za uchochezi tu,na tayari msajili wa magazeti ameshaawaandikia barua wahariri wamegazeti hayo lakini bado wanakuwa wabishi wanaendelea kuandika habari tofauti kuhusu bunge la Katiba”alisema Mpashaji huyo wa habari kutoka wizara ya habari.
Chanzo hicho kilizidi kusema Gazeti la kila siku la Nipashe limeonywa sana ili wahariri wake wamekuwa wakimkaidi msajili wa Magazetii,baada ya kuandikwa Barua ya kuonywa na Msajili wa Magazeti lakini bado wamekuwa wakibisha.
Mwandishi wa Mtandao huu alishuhudia Barua aliyoandiwa Mhariri wa Gazeti la Napashe kutoka Msajili wa Magazeti Raphael Hokororo yenye kumbukumbu namba 77/319/01/80 ambapo barua hiyo ilikuwa na kichwa cha Habari Habari uliyochapisha inayohusu Bunge la Katiba,katika barua hiyo msajili alitoa malalamiko yake kwenye gazeti hilo toleo 15 Sepmtemba 2014 toleo namba 0578237 uliochapisha Habari iliyosemeka “BUNGE LA KATIBA HASARA”
Habari hiyo ilizidi kusema Mabilioni yake yangetosha kujenga Zahanati 600,na Noti zake zikipangwa barabarani ni Dar mpaka Bukoba,ambapo Msajili wa Magazeti nchini amemtaka Mhariri wa Gazeti hilo kwenda kutoa maelezo kwa madai bunge hilo lipo kisheria.
Kwa upande wake Gazeti la Mawio nalo liko katika njia panda kutokana na wakati wowote nalo litafungiwa kutokana na Gazeti hilo kutofahamika wamiliki wake haswa,
Kwa mujibu wa Mpashaji wetu aliyoka ndani ofisi ya Mkurugenzi wa Habari Maelezo ambaye akutaka jina lake kutajwa kwenye Mtandao huu alisema Serikali hususani ofisi ya Msajili wa magazeti imefanyiwa rafu sana katika uanzishaji wa Gazeti la Mawio.
“Nahilo gazeti la Mawio sikufichi lina mda mfupi sana na lazima litafungiwa mda wowote,kwasababu serikali imeshajua hilo gazeti wamiliki wake ni walewale waliokuwa wanamiliki gazeti liliofungiwa na serikali kwa mda usiojulika la mwanahalisi,kwasababu gazeti la Mawio wamiliki wake pamoja na Mhariri wake sio wanaotambulika na ofisi ya msajili wa Magazeti”
“
Na tunajua kwamba gazeti hilo linamilikiwa na Mtu mmoja wa Fedha kutoka chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na Mhariri wa gazeti la Mwanahalisi Saed Kubenea,na wale ambao msajili inawatambua sio hawa wanaomiliki gazeti,kwasabu wamiliki wa mwanzo wa gazeti la Mawio bila kuleta taarifa kwa msajili na wanajua wakileta msajili atawakatalia kutokana na hao wakina kubenea kujilikana kwa uchochezi”alisema Mpashaji huyo wa Habari
Kwa upande wa Gazeti la Tanzania Daima nalo lipo wakati wowote kufungiwa kutokana na kile anachokiita msajili wa Magazeti nchini ni kuwa linaandika habari za upotoshaji,
Gazeti hilo linashutumiwa kutokana na Vichwa vya Habari wanavyoviandika ambavyo ofisi hiyo ya Msajili inaviona ni vya kichochezi nitoleo namba 3554 la Agosti 27, 2014 na toleo namba 3555 la Agosti 28, 2014 tulikuwa na habari zenye vichwa: Kikwete anywea na Kikwete ‘alamba matapishi’ yake, na Rais Kikwete Anywea
Ndipo msajili wa Magazeti nchi alitaka gazeti la Tanzania daima kuomba Radhi kwa uzito ule ule wa Mwanzo na gazeti hilo likafikia uamuzi huo na kuomba Radhi kwenye machapisho yake,Licha gazeti hilo kuomba Radhi lakini bado gazeti hilo linawindwa na mda wowote litafungiwa na serikali kutokana habari zake ambazo zinagusa maslai ya Serikali.
Kupewa Vitisho hivi kwa wamiliki wa Magazeti nchini,pamoja na Wahariri,kunaendana na sawa na kauli aliyosema Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari Joseph Mbilinyi “SUGU” wakati anawasilisha Makadilio ya bajeti ya Wizara hiyo ya Habari bungeni ya Kambi ya Upinzani,alisema
“Kwa sasa zipo fikra miongoni mwa wadau wa vyombo vya habari kwamba uhuru wa habari nchini unazidi ‘kuwambwa msalabani’ kwa sababu ya utatu wa hatari ambao umetengenezwa na Serikali ya CCM, kwenye Wizara ya Habari, Vijana, Michezo na Utamaduni. Utatu huu hatari unaundwa na waziri mwenyewe Dk. Fenela Mkangara ambaye mbali ya kwamba si mwanahabari, si mwanasanaa, si mwanamziki wala si mwanamichezo, taarifa zinaonesha kuwa amekuwa na dhamira ya kupambana na vyombo vya habari, ambao ni wadau wake, tangu alipoteuliwa.”
Hotuba hiyo ilimnukuu mmoja wa waandishi waandamizi nchini, ambaye aliandika haya kuhusu huyo Waziri;
“Waziri mwenye dhamana Dk. Fenella Mukangara kwa muda mrefu amekuwa na nia ovu dhidi ya vyombo vya habari. Julai mwaka jana (akimaanisha 2012) tukiwa Hoteli ya Dodoma mjini Dodoma, wakati tunafanya mazungumzo rasmi na Waziri Mukangara, walikuwepo Theophil Makunga, Pili Mutambalike, Neville Meena na marehemu Alfred Mbogola na wengine, Dk. Mukangara alitoa kauli iliyotushtua wengi na sasa ndipo tunaona inatekelezeka kwa vitendo.”
Mwandishi huyo aliongeza kwa kunukuu maneno ya Waziri Mukangara ambaye amenukuliwa akisema;
“Nikipata fursa Mwananchi nitalifuta, mimi linanikera sana. Tena na Nipashe nao naona wanakuja, ikibidi nitawafungia tu, mimi siogopi kitu.” Hayo ni maneno ya Waziri anayetakiwa kuwa mlezi wa vyombo vya habari!
Mwandishi huyo katika makala yake akaendelea kuandika hivi;
“Baada ya kauli hii tuliendelea na mazungumzo mengine, lakini Meena akatuambia kuwa Dk. Mukangara aliwahi kutoa kauli kama hii ofisini kwake walipokwenda akina Jesse Kwayu, Meena na Absalom Kibanda kuomba Gazeti la Mwanahalisi lifunguliwe. Mwanahalisi alilifungia kwa muda usiojulikana…”.
Hizi ni tuhuma nzito sana kuweza kukaliwa kimya na Serikali yoyote makini. Ni jambo la ajabu kuwa pamoja na uzito wake, si tu kwamba hazikupata majawabu yanayostahili, bali hazikujibiwa kabisa. Anayebeba tuhuma hizo hadi leo anakaa meza ‘moja’ na Rais wakati wa vikao vya Baraza la Mawaziri.
Katika kukamilisha hoja ile ya utatu wa hatari, hotuba ile ya Kambi ya Upinzani, ikaendelea kusema;
“Si Waziri Mukangara mwenyewe wala mtu mwingine yeyote kwa niaba yake, amewahi kukanusha maneno hayo aliyonukuliwa akiyasema hadharani mbele ya wadau ambao yeye anapaswa kuwa kiongozi na mlezi wao. Kutokana na mwenendo wa Waziri Mukangara wa kupambana na vyombo vya habari, unaofumbiwa macho na mamlaka iliyomteua, labda kwa bahati mbaya au sehemu ya mkakati wa serikali hii ya CCM. Uhusiano wa waziri na vyombo vya habari ulifikia hatua mbaya zaidi, baada ya wadau wa habari waliokutana Oktoba 9 mwaka jana, kufikia maazimio kadhaa, ikiwemo lile linalosema;
“Kusitisha kuandika, kutangaza na kupiga picha shughuli zozote zitakazowahusisha au kuratibiwa na Mheshimiwa Fenella Mukangara na Assah Mwambene hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo. Adhabu hiyo inaanza mara moja kuanzia leo.”
Hotuba ikaongeza;
“Hapo juu kwenye moja ya maazimio ya wadau wa habari, ametajwa Assah Mwambene, huyu ni Mkurugenzi wa Habari Maelezo. Mkurugenzi huyu ambaye amewahi kufanya kazi kwenye vyombo vya habari kama mwandishi, pamoja na kwamba kwa majukumu yake hayo alipaswa kuwa mtu wa karibu kama mwelekezi na kiongozi kwa wadau wake (au wenzake), kwa kushirikiana na Waziri Fenella Mukangara, amekuwa ni mwiba kwa utendaji wa vyombo hivi, akihusika kuuweka uhuru wa habari na uhariri katika sintofahamu kubwa.
“Kitendo cha Mkurugenzi wa Habari Maelezo kufanya maamuzi makubwa ya kuyatisha magazeti ya Mwananchi na Rai, kutimiza wajibu wa kuendelea kuhabarisha, kwanza bila kuwa na msingi wowote wa kisheria na pili bila kuwasiliana na wakubwa wake wala wasaidizi wake, kama ilivyotamkwa na aliyekuwa Naibu Waziri Amos Makala, ni jambo ambalo linathibitisha jinsi alivyo sehemu ya utatu huu tunaozungumza hapa

No comments:
Post a Comment