Meneja wa udhibiti wa viwango kutoka baraza la habari Tanzania akizungumza na wanahabari mapema leo kuhusu mchakato wa tuzo za umahiri wa uandishi wa habari nchini Tanzania |
Baraza la habari Tanzania leo wametangaza rasmi
kuanza kwa mchakato wa tuzo za umahiri wa uandishi wa habari Tanzania mashindano
ambayo yatakjuwa ni mara ya sita kufanyika nchini Tanzania.
Akizungumza na wanahabari leo jijini dare s salaam Meneja wa udhibiti wa viwango kutoka baraza la habari MCT Bi PILI MTAMBALIKE amesema kuwa katika mashindano ya mwaka huu kuna mabadiliko
kidogo ambapo amesema kuwa kuna makundi ambayo yameongezwa katika nafasi
zinazoshindaniwa ambayo ameyataja kuwa ni gesi,mafutana uchimbaji madini na
kundi la afya ya mama na mototo.ambapo amesema kuwa makundi hayo yameongezwa
kutokana na umuhimu wake hapa nchini kwa sasa.
Tamasha hilo ambalo limepangwa kufanyika mwaka
mwakani mwezi wa tatu tarehe 24,2015 ambapo mtambalike amesema kuwa tuzo hizi
zinalenga kuwatambua na kuwatunza waandishi wa habari waliofanya kazi yao
vizuri katika kazi zao na makundi mbalimbali kushindaniwa
Mmoja kati ya waratibu wa shindano hilo Bi CHIKU LWENO akiielezea mikakati ya tuzo hizo kwa msimu huu |
Makundi yatakayoshindanishwa mwaka huu ni uandishi
wa habari za uchumi,habari,michezo na tamaduni,mazingira,afya,watoto,HIV/UKIMWI,utawala
bora,jinsia,sayansi na technologia,afya ya mama na motto,uchunguzi,elimu,watu
wenye ulemavu,utalii na uhifadhi,mpiga picha gazeti,mpiga picha runinga,mchora
katuni bora,uandishi wa habari za kilimo,afya ya uzazi kwa vijana,pamoja na
tuzo ya uandishi wa habari za gesi,mafuta na uchimbaji madini,pamoja na kundi la
wazi.
Bi PILI MTAMBALIKE amewataka waanndishi wa habari
kujitokeza kwa wingi kupeleka kazi zao ili zishindanishwe na kupata mshindi wa
tuzo hizo.
No comments:
Post a Comment