Friday, October 24, 2014

KITENDAWILI CHA KATIBA MPYA CHATEGULIWA--TUME YA UCHAGUZI YAWEKA WAZI TAREHE YA KURA YA MAONI

Kile kitendawili ambacho kilikuwa kinawasambua wadau mbalimbali wakiwepo vyama vya siasa, asasi za kiraia na wananchi kwa ujumla wake kimeanza kupata majibu yake kutoka tume ya taifa ya uchaguzi NEC kwa kusema kuwa wananchi wote watakuwa tayari wamejiandikisha katika daftari la kudumu Tanzania nzima ifikapo 18th April kwakani,

             Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo kuhusiana na sakata hilo,Jaji mkuu mstaafu wa Zanzibara Mh. Hamid Mahamoid Hamid amewatoa hofu waTanzania kwa kusema kuwa hakuna mwananchi ambaye anastahili kupiga kura akashindwa kufnya hivyo kwani tayari wanauhakika wa asilimia zote kuwa ifikapo Apr 18 tayari zoezi hilo litakuwa limekamilika,

     Jaji huyo ameendelea kusema kuwa Tayari wameshaanza kupokea fedha kutoka serikalini ambapo jumla ya shilingi Bilioni 15 Tayari zimeshapokelea tayari kwa zoezi hilo ambalo linatarajiwa kukamilika kwake mapema hiyo April.


             Jaji Hamid ameongeza kusema kuwa tume yake inauhakika wa kuendesha zoezi hilo bila kukwama kwani wanakila kitu ambacho kinatakiwa katika kukamilisha usajiri huo wa wapiga kura kwa kutumia BVR

    Kauli ni kama kumuunga mkono rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambaye hivi karibui aliukuliwa kuwa zoezi la kupiga kura ya maoni litakuwa mwezi wa nne, bila kubainisha tarehe rasmi ya kufanyika katika mwezi huo,
Rais aliweka wazi nia ya kupiga kura yamaoni kuhusu katiba pendekezwa mapema hivi karibuni,

          Akizungumzia changamoto ambazo huwenda zikawa kikwazo kwa mustakabali wa maendeleo ya zoezi hilo, Hamidi amesema wanajua kuna changamoto mbalimbali zitaikumba mchakato huo, lakini wamejipanga vizuri kukabiliana na changamoto hizo,

      Ikumbukwe kuwa mchakato huo wa kuandikisha wapiga kura katika Daftari la kudumu linahitaji umeme wa uhakika kwani zoezi lote linendwa kwa kutumia mitambo, akifafanua jinsi walivyojipanga na changamoto hiyo ya umeme,
Jaji Hamidi amesema tayari juhudi mbalimbali zimeshachukuliwa ikiwamo kutumia mitambo ya sola, Majenerator, na vyanzo vingine vya umeme ambavyo wanajua havitawasumbua katika zoezi zima,

       Aidha jaji huyo ameongeza kusema kuwa tayari wameanza mchakato wa kuchukuwa power server katika vituo vyote ambavyo zoezi linafanyika ili hata umeme wa Tanesco ukikatika basi kutakuwa na njia mbadala ya kutumia ili zoezi liendelee kama kawaida,

     
Tunajua wazi kuwa umeme wa Tanesco ni Tatizo lakini tumejipanga kuhakikisha kuwa hatupati changamoto kama hiyo na hivyo kuweza kuchelesha mchakato wa kukamilika kwa daftari la kudumu la mpiga kura,

No comments: