Historia kubwa imewekwa muda huu hapa viwanja vya jangwani jijini dar es salaam Tanzania Ambapo vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi ukawa muda huu wamesain mkataba ambao unawafanya wao sasa kuungana na kuzungumza lugha moja ya kuhakikisha kuwa wanafika mbali zaidi wakiwa pamoja,umoja huo ambao unaundwa na CHADEMA,CUF,NCCR MAGEUZ pamoja na NLD muda huu wamesaini kwa pamoja makubaliano hayo mbele ya wanachama wao maelfu waliojitokeza katika viwanja hivyo hapa jijini dar es salaam. Akizungumza na wanachi waliojitokeza hapa katibu mkuu wa chadema aesema kuwa makubaliano hayo sio makubaliano ya vyama na viongozi wakuu bali ni makubaliano ya wanachi wote ambao wanapenda haki na amani ya tanzania. mtu wangu hapa kuna picha za shuguli hiyo ya kusaini makubaliano hayo na tutazidi kukupa kile kinachojiri hapa uwanja wa jangwani. |
No comments:
Post a Comment