Saturday, November 29, 2014

FILAMU YA ESCROW YAMALIZIKA,HAYA NDIO MAAZIMIO MAPYA NANE YA BUNGE

Mwenyekiti wa PAC Zitto Kabwe amesoma maazimio mapya ya Bunge kwa mujibu wa kamati maalumu iliyoundwa leo na kuhusisha CCM, PAC na UKAWA

Azimio: Mamlaka ya uteuzi iwawajibishe na inashauriwa kutengua uteuzi wa Waziri wa Nyumba, ardhi na makazi Prof Tibaijuka, Waziri wa Nishati na Madini Prof Muhongo, Mwanasheria Mkuu wa serikali Jaji Werema, na Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Maswi

Azimio: Bunge liwawajibishe wabunge ambao ni sehemu ya bodi ya TANESCO na viongozi wa Kamati za Bunge

Azimio: Mamlaka husika ziitangaze Benki ya Stanbic, Mkombozi na benki yoyote nyingine itakayogundulika kuwa zinahusika na utakatishaji wa fedha haramu

Azimio: Kwa kuwa majaji walihusika, Rais aunde Tume ya kijaji ya uchunguzi na kuwasimamisha jaji Mujulusi na Prof Luhangisa


Azimio : Serikali ipitie upya mikataba ya Umeme na itoe taarifa kabla ya kumalizika kwa mkutano ujao wa bunge la Bajeti

Azimio : Serikali ichukue mitambo ya IPTL na iikabidhishe kwa TANESCO

Azimio: TAKUKURU na Polisi wamchukulie hatua bwana Sethi, na kumfungulia mashitaka akithibitika

Wasira: Tuamini kwamba haya yote ni kwa maslahi ya watanzania, CCM imeshirikiana na kambi ya upinzani kufanya maamuzi sahihi

Spika awahoji wabunge, na wao wamepitisha azimio la bunge kama lilivyosomwa na @zittokabwe

No comments: