TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
JESHI
LA POLISI KANDA MAALUM LATOA TAHADHALI KWA WANAWAKE KUTOSHIRIKI KIMAPENZI NA
WATU WASIOWAJUA
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linatoa tahadhari kwa wanawake wa jiji la
Dar es Salaa hususani wasichana kuwa makini na wanaume wanaowataka kimapenzi na
baadaye kuwauwa na kutelekeza miili yao.
Zimekuwepo
taarifa juu ya kuwepo kwa wanaume wawili wanaoshawishi wanawake kuwa nao
kimapenzi na baada ya muda huwauwa. Hivyo natoa tahadhari kwa wanawake wa jiji
la Dar es Salaam kuchukua tahadhali juu ya watu hawa maana huatarisha maisha
yao au ya familia zao.
Inaaminika
watu hao huwashawishi akina dada au wanawake kwa jumla ili wawe nao kimapenzi
huku wakiwasaidia kwa huduma mbalimbali za kimaisha na kisha kuwauwa.
Natoa
wito kwa wanawake wote kutokukubali kushawishiwa kirahisi na wanaume wasiowajua
ambao wanataka kuwa nao kimapenzi na starehe kwani kwa kufanya hivyo wanaweza
kuingia katika mtego mbaya na pengine hata kuyaweka maisha yao rehani.
Aidha,
katika siku za hivi karibuni yameripotiwa matukio kadhaa ya mauaji ya aina hiyo
ambapo kwa sasa wanawake wapatao sita tayari wamepoteza maisha. Haijafahamika
madhumuni ya wauaji hao na huenda ni mambo ya ushirikina n.k.
Msako
mkali unaendelea ili kuwabaini na Jeshi la Polisi Kanda Maalum linatoa wito kwa
wakazi wa jiji la Dar es Salaam kutoa taarifa sahihi kwa Jeshi hilo na vyombo
vingine vya usalama ili kuwabaini na kuwakamata ili sheria ichukue mkondo wake
dhidi ya wahusika.
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment