Maafisa wanaojitambulisha kuwakilisha Kampuni ya Pan Africa Power-PAP wapo mahakama kuu ya Dar es salaam kufungua shauri la kuzuia suala la Escrow kujadiliwa na Bunge.
PAP wamefungua shauri hilo kwenye mahakama kuu kanda ya Dar es salaam wakimshitaki waziri Mkuu, Spika wa Bunge, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG na katibu wa bunge kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa wakati kwa jambo lililokwisha kutolewa hukumu na mahakama na kukaguliwa na hivyo kutaka kuzuia mjadala wowote wa suala hilo hadi ufafanuzi wa mahakama utakapotolewa.
Kufuatia suala la maafisa wanaojitambulisha kuwakilisha Pan Africa Power-PAP kuwepo mahakamani kufungua shauri la kuzuia suala la Escrow kujadiliwa na Bunge Spika Mheshimiwa Anne Makinda amesema hakuna mtu anayeweza kuzuia bunge kufanya kazi za kibunge.
Alitoa kauli hiyo baada ya wabunge kuhoji juu ya taarifa hiyo ya PAP Kufungua shauri na kusema kuwa Bunge lina Kinga ya kutoingiliwa hivyo Ripoti ya CAG itagawiwa kwa wabunge wakati wa mchana kwa maandalizi ya mjadala wa Escrow.
No comments:
Post a Comment