Imeandika na Josephine B Mramba
Dondoo Kutoka Kikao cha Ndani ya Baraza la Mawaziri kilichofanyika jana Dodoma kilichofanyika Ofisi za TAMISEMI.
Kikao rasmi cha kujadili sakata la IPTL/ESCROW namna wahusika watakavyowajibishwa au kuokolewa.
1.Misimamo ya Mawaziri tofauti tofauti.
Mwigulu Nchemba ambaye ni Naibu waziri wa Fedha anatajwa kuwa Waziri wa kwanza kuonesha msimamo wake wazi wazi kuwa Sakata la IPTL/ESCROW ni hujuma dhidi ya Uchumi wa Nchi.acharuka,AAGIZA MALI ZOTE NA PESA ZOTE ZILIZOLIWA, ZILIZOTAWANYWA ZIKAMATWE.Naibu huyu ambaye mara kadhaa amekuwa akitajwa na vyombo vya habari kwa juhudi zake za kuokoa matumizi mabaya ya fedha na hata Watanzania wengine kuamua kumbatiza jina la Sokoine wa pili ikiwa ni kufuata nyayo za aliyewahi kuwa Kiongozi Makini Nchini hayati Moringe Sokoine.
Mwigulu ndani ya kikao hicho cha siri anatajwa kuendeleza ujasiri wake kuhusu mambo yenye masilahi ya Taifa. Wakati watu na tetesi mbalimbali zilikuwa zinaongelea kujiuzulu, Mwigulu amejitokeza kwenyw kikao hicho na kusema CAG ameshamaliza utata, sasa mali zote, fedha zote za IPTL zikamatwe na wahusika wote wakamatwe.
Nanukuu kama nilivyosikia"Tumezoea kusema eti tumewajibisha watu kwa wao kujiuzuru, "Kujiuzuru ni kupewa Likizo ya kwenda kula fedha ulizo ziiba"anasema Mwigulu, Hili ni jambo la mazoea, sasa, CAG ameshasema pesa zile zilikuwa mali ya umma, sasa zikamatwe zote, na wahusika wote wakamatwe"
Mwigulu alienda mbali zaidi na kusema hata ambao walishastaafu na wamehusika kulihujumu taifa wakamatwe na akaunt zao zikamatwe, zifilisiwe zirudishwe kwa wananchi.
Katika hatua nyingine Naibu huyo anayeshughulikia mambo ya sera, Mwigulu ameagiza mtumishi wa TRA aliyepewa 1.6bilion afukuzwe kazi, akamatwe, na akaunti ifilisiwe fedha irudi serikalini. Pia mitambo ya IPTL ikamatwe irudishwe serikalini. Utamaduni wa watu kujiuzulu na kuhesebu kuwa ni adhabu ni jambo la zamani, sasa ili kukomesha wizi, uzembe na ufisadi sasa tuwakamate wahusika wote, tuwafilisi na tuwaweke ndani na tuwafunge.
Habari za uhakika kutoka kikao cha baraza la Mawaziri zinasema, jana Mwigulu Nchemba aliongea kwa sauti ya mamlaka mbele ya Waziri mkuu nakusema kujiuzuru sio adhabu stahiki kwa wizi Mkubwa kama huu wa Mali ya Umma,Hisia hizo zikiwa zimegubikwa na maisha yake halisi ya umasikini aliyokulia na huku akihusisha Wizi wa fedha na hujuma dhidi ya Watanzania Masikini.Mbunge huyo wa iramba anasisitiza kwa kusema " Tazama wanafunzi, watoto wa masikini zaidi ya elfu 40 wamekosa mikopo, madawa hospitalini hakuna masikini wanakufa, watu wasio na hatia wanafungwa kwa kukosa michango ya maabara, walimu wanadai, wazabuni wanauziwa nyumba zao na mabenki huku wakiidai serikali kwa huduma walizotoa, leo wezi tuwape adhabu ya kujiuzuru? Tuwape likizo ya kwenda kutumia fedha walizo waibia masikini? Hapana, "Enough is enough" ndg Waziri mkuu tuwakamate, tuwafilisi, tuwafunge. Pesa na mali virudi serikalini."
Kwa yule mtumishi wa TRA aliyekula fedha za IPTL zaidi ya 1.6 B,Mwigulu akatoa agizo kuwa "Nimemwagiza kamishna wa kodi amfukuze kazi yule wa TRA iliyoko chini ya wizara yangu, na afilisiwe, pia mitambo na kodi vikamatwe, na wahusika wakamatwe. Hatuwezi kuendeleza mazoea ya kufunga masikini na kuwapa likizo wezi wakatumie fedha. Walio serikalini na walioko kwenye siasa wakamatwe na tuwafilisi fedha irudi serikalini."
Taarifa za uchunguzi zunasema tayari TRA imechukua hatua."
Naibu Waziri KILIMO Mh.Godfrey Zambi wanusurika Kukunjana na Werema(Mwanasheria Mkuu wa Serikali).
Wakati kikao kikiwa kimepanda joto la juu,Mawaziri wakifikia makubaliano kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na madini Maswi na Mawaziri waliohusika ni lazima waachie ngazi,Ndipo Werema alipotaka kumkunja Mh.Zambi baada ya kutoleana maneno machafu dhidi ya mali ya uma.
Madai yanakwenda mbali kuwa,Zambi alikuwa anapigia kelele kuwa inawezekanaje Mwanasheria mkuu kubariki wizi wa Fedha za Umma?.Ni wapi watu wa msoma wakasifika kwa wizi wa mali za Umma?.Chokochoko hizo ndio zilipelekea Ugomvi kati ya Zambi na Werema.
Mbali na Mawaziri hao,Mh.Tibaijuka amekuwa Mwizi wakwanza wa IPTL kukubali kuwajibika katika sakata hili mbele ya kikao cha baraza la Mawaziri.
Ni wakati Muafaka sasa kwa Watanzania wote kuunga kupaza sauti kama akina Zitto walivyofanya,Kuunga mkono zaidi Machozi ya akina Mwigulu waliojitolea kutetea Masikini wakati huo huo wanahujumiwa na Mawaziri wenzao ndani ya Chama tawala,Mwigulu ameanua kujilipua Mzima mzima bila kujali yeye ni nani ndani ya Chama kwa Malengo kuwa CCM haipo tayari kukumbati waovu na wezi.
|
No comments:
Post a Comment