Chama cha
wananchi CUF leo muda huu kimewataka waziri mkuu wa Tanzania mh MIZENGO
PINDA,mwanasheria mkuu wa Tanzania jaji Fredrick werema,waziri wa nishati na
madini profesa SOSPETER MUHONGO,pamoja na katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini bwana ELIAKIM MASWI kuachia
ngazi mara moja au kufukuzwa kazi kutokana na wao kuonekana wazi kuwa
wanautetea ufisadi wa mabilioni ya escrow unaoendelea nchini.
Akizungumza na wanaandishi wa habari mapema leo
makao makuu ya chama hicho mwenyekiti wa CUF profesa IBRAHUIM LIPUMBA amesema
kuwa viongozi hao wamekuwa mstari wa mbele kuonyesha wazi kuwa hawako tayari
kuona wahusika wa ufisadi huo wakiadhibiwa hivyo hawana sifa ya kuendelea
kuiongoza nchi kwani hawana maslahi kwa wanachi huku akiitaka TAKUKURUI nao
kuwachunguza viongozi hao kama wanahusika na ufisadi huo.
Hapa akizungumza na wanahabari |
“hivi karibuni tulimsikia waziri mkuu akiwadnaganya
watnzania kuwa fedha zilizopo kwenye account ya tegeta ESCROW sio mali ya umma
bali ni mali ya kampuni binafsi kauli ambayoni ya uongo na yakujaribu kuficha
maudu hayo”amesema lipumba
Aidha CUF wameitaka TAKUKURU kuwakamata mara moja
vigogo JAMES RUGEMALIRA ambaye mtandao huu pia umesharipoti kuhusika kwake
pamoja na HARBINDER SINGH SETH na kuwafungulia mashtaka ya rushwa mna wizi wa
mali ya tanesco kwani hawa ndio wahusika namba moja wa kuzigawa pesa hizo kama
zao.
Aidha lipumba ametaka pia mkuruygenzi wa tanesco
pamoja na bodi nzima ya tanesco kufutwa mara moja kwa kuwa haikutimiza wajibu
wake wa kulinda maslahi ya shirika wanaloliongoza.
Katika hatua nyingine chama hicho kmesema kitafanya
maandamano ya nchi nzima baada tu a mjadala huo kumalizika bungeni
kuwashinikia viongozi waliohusika kuwajibika na pia kuwapongeza wabunge
waliosimamia kuonyeshwa kwa ufisadi huo.
No comments:
Post a Comment