
Mhe Zitto kabwe
kauli ya kwanza inatoka kwa kada huyu
Naitakia kamati ya PAC kila la kheri katika kuchambua na kuhoji kila
aliyetajwa katika Ripoti ya CAG kuhusu ukwapuaji wa Mabilioni kutoka
akaunti ya ESCROW
Kampeni yetu ya "IPTL-BRING BACK OUR MONEY" imepata ushindi Mwingine
Wale wote wanaohoji iweje tuungane na Zitto na Kafulila katika mapambano haya wanalengo moja tu,Divide and rule.
Wanataka kutumia mwanya fulani kufifisha vita hii
Inafurahisha sana Gazeti la Serikali la Habari Leo Wiki iliyopita
kuchapisha makala za kuonyesha mashaka juu ya nguvu na ushirikiano wa
ghafla kwenye suala hili
Nimejiuliza ni lini Gazeti la Habari Leo liliwahi kuwa na uchungu au nia
njema na Upinzani hadi litilie mashaka ushirikiano wetu na akina Zitto
na Kafulila kwenye suala hili
Wanafanya kazi ile ile tuliyosema,Ya kupotosha.
Kampeni hii inaratibiwa na kundi kubwa bila kujali itikadi zetu
Najua tupo katika vita kubwa sana na adui atatumia kila mbinu ili apumue.Tutashinda
Kamwe hatutayumba katika vita hii hadi tone la Mwisho
Katika vita hii sina adui wala rafiki wa kudumu bali ajenda ya kudumu,Maslahi ya Tanzania.
"
If you fight indignation at every injustice then you are a comrade of mine-Mwanamapinduzi Che Guevara.
PAC nawatakia kila la Heri,Hongereni washirika wote katika vita hii
Aluta continua,Victory Ascerta...!
KAULI YA TATU INATOKA KWA MWANDISHI WA HABARI
No comments:
Post a Comment