Wafanyabiashara wa soko la Machinga
Complex wameibuka na kulaani hoja binafsi iliyowasilishwa bungeni N a
mbunge wa Jimbo hilo, Ndg. Musa Zungu na kusema kuwa hoja hiyo imelenga
kuwafanya wafanya biashra wa soko hilo kuendelea kuwa masikini huku yeye
akifaidika na maslahi yake mwenyewe,
Akizungumza na Mtandao huu mapema hii
leo, Kaimu mwenyekiti wa Soko hilo Ndg. Gerald Mpagama amesema
wafanyabiashara wa soko hilo wanalaani hoja hiyo,
SISI wafanyabishara wa soko hili la
Machinga complex tunalaani vikali hoja binafsi iliyotolewa na mbunge
wetu kuwa eti Mkurugenzi wa jiji hili la Dar es Salaam akisaidiana na Mkuu
wa mkoa huu wanashiriki kusababisha vurugu za wamachinga bila sababu za
msingi na kusema kuwa hoja hiyo imelenga kumjenga yeye kisiasa huku
wafanyabishara wakiumia,
Ameendelea kusema kuwa kama kweli Zungu
alikuwa na uchungu na wafanyabiashara, kwa nini asingewashirikisha
katika kupeleka hoja hiyo, na badala yake tunaona ameibuka kutoka
kusikofahamika nakuibua hoja ambayo ni kandamizi kwa walala hoi wa soko
la machinga complex,
Kwa kweli Zungu ametusikitisha sana,
hata kama ndiyo utawala lakini hakuna utawala wa mabavu kama anavyofanya
ayeye, Tunafahamu serikali ya JK ni sikivu na ndio maana akaletwa
mkurugenzi ambaye anaijua kazi yake vizuri lakini watu wachache
wanalenga kumuangusha, aliongeza Bwana Mpagama.
No comments:
Post a Comment