kaimu naibu katibu mkuu ambaye pia ni mkurugenzi wa mipango na uchaguzi SHAWEJI MKETOakionyesha barua ambayo wamemwandikia waziri mkuu juu ya rafu za uchaguzi |
Ikiwa kesho ndo siku ya uchaguzi wa serikali za
mitaa kufanyika nchini tanzaniachama chawananchi CUFleo kimesema kuwa
kimemuandikia waziri mkuu pamoja na wizara ya tamisemibarua rasmi ya malalamiko
juu ya rafu mbalimbali zinazochezwa juu ya wagombea wa chamachao pamoja na
UKAWA kwa ujumla.
Akizungumza na wanahabari mapema leo makao makuu ya chamahicho kaimu naibu katibu
mkuu ambaye pia ni mkurugenzi wa mipango na uchaguzi SHAWEJI MKETO amesema kuwa
kuna udhibitisho kuwa CCM kwa kushirikiana na serikali wamejiandaa
kuvurugauchaguzi huo ili kupora ushindi ambapo amesema kuwa mkakati huo
umeonekana wazi baada ya wagombea wengi wa UKAWAkuenguliwa katika kinyanganyiro
hicho.
Amesema tukio la jana lililotokea mabibo jijini dare s salaam ambapo
kura zaidi ya 500 zilikutwa zikichapishwa kwa ajili ya kutumika huko kilosa ni
tukio ambalo limeonyesha wazi kwa hakuna mwenye nia ya dhati kulisaidia taifa
kwani kinachofanyika ni wizi na wao kama chama hawawezi kuvumilia.
Aidha akizungumzia matumizi mabaya ya nguvu za dolakatikachaguzi
amesema kuwa jana wilayani tandahimba kata ya lokokoda wanachama wa cuf wapatao
wanne walikamatwa na wanajeshi wa jeshi la wananchi JWTZ wakiwa wamewafuata
majumbani kwao ambapo baada ya kuwakamata waliwaingiza katikakarandinga ambalo
lilikuwa na sakari zaid ya 50 na kuwapeleka katika kambi ya jeshi ya
naliendelele iliyopo mtwara ambapo askari wawili kati ya hao walianza kuwapiga
kwa madai kuwa wameficha mabomu majumbani kwao,ambapo baadae kiongozi wa msafara
aizuia wasipigwe na kuwapatia magodoro wakalala hadi asubuhi na kuwapeleka
katika kituo cha polisi na kuwaacha kwa OCD kwa mahojiano.
Amesema kuwa matendo haya hayaji kwa bahati mbaya
kwani yanalenga kuwadhoofisha wanachama na wanachi ili wasijitokezekwawingi
katika vituo vya kupiga kura ilikuwachagua viongozi wanaowataka.
Cuf
wameitaka
serikali kuacha mara moja jaribio la kuingiza nchi katika machafuko yasiyo na
tija kwa kuwawatanzania ni watu wa amani na amani yetu haiwezi kuchezewa na
watu wachache kwa tamaazao zamadaraka.
No comments:
Post a Comment