Na karoli Vinsent
SIKU chache kupita baada ya Wamiliki wa Viwanda vya Sukari nchini kusema viwanda Vyao viko hatarini kufa kutokana na serikali Kuendelea kuagiza sukari ya nje ya nchini na kupelekea Sukari ya ndani kukosa soko na kuvifanya Viwanda hivyo kupunguza wafanyakazi .
Naye Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza, Mb Ameibuka na kusema Kamwe Serikali haitoacha kuagiza Sukari nje nchi kutokana na Viwanda Vilivyopo nchini kukosa uwezo wa kuzalisha Sukari za Matumizi ya Viwandani kwani Viwanda vya ndani vinauwezo wa kuzalisha sukari za majumbani peke yake.
Pia Waziri Chiza Akasema Tatizo ambalo Serikali linakumbana nalo ni Uingizaji wa Sukari Kinyemela kutoka nje ya nchini ambao ndio limekuwa kikwazo katika Viwanda hivyo.
Waziri Chiza ameyasema hayo Leo Jijini Dar es Salaam Wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari,aliouitisha mahususi kuzungumzia hali ya Sukari nchini,ambapo pamoja na Mambo mengine Waziri Chiza alisema Wamikili wa Viwanda vya Sukari wanashindwa kusema Ukweli kwa Umma,kwani sababu ya Sukari zao kujazana kwenye Maghala inatokana na Viwanda hivyo kuzalisha Sukari zenye matumizi ya Majumbani na sio Viwandani.
“Tazito hili la kulundikana kwa sukari na kukosekana wateja wasizingizie Sukari zinazotoka nje ya nchi,kwani tatizo la sukari limetokana na Viwanda vya sukari vya ndani haiviwezi kuzalisha Sukari kwa ajiri ya matumizi ya Viwandani na Viwanda vinavyoitaji Sukari vinalazimikia kuagiza Sukari nje ya nchini ,na wasipofanya hivyo Viwanda haviwezi kuzarisha bidhaa,na ndio inatufanya tuagize sukari nje nchi”alisem Waziri Chiza.
|
Waziri Chiza aliongeza kuwa Kinachotakiwa kwenye Viwanda hivyo sio kulalamika kwenye vyombo vya Habari kwani hoja ya Waziri kuzuia kuto Vibari kwa Waingizaji wa Sukari ni kuudanganya Umma kwani Vibari hivyo vinatolewa na Bodi ya Sukari nchini na kushirikiana na Taasisi mbalimbali na sio Waziri wa huyo.
Aidha,Waziri Chiza aliongeza kuwa kwa sasa hali ya uingizaji wa Sukari kwa magendo imekuwa kubwa sana na ndio sababu inayofanya hata Viwanda vya ndani kushindwa kushindana na Sukari hizo kwenye soko la nchini.
Pia Waziri Chiza akasema kwa sasa anashirikiana na Mamlaka za Ulinzi wanchi kupambana na Waangizaji wa Sukari kimagendo kuhakisha wanachukuliwa hatua
No comments:
Post a Comment