Kuelekea uchaguzi wa serikali
za mitaa nchini Tanzania
uchaguzi unaotarajiwa kufanyika siku ya jumapili ya mwisho wa wiki hii,kituo
cha sheria na haki za binadamu LHRC leo kimetangaza kufanya uangalizi wa
uchaguzi huo kwa njia ya TEHEMA yaani ICT-election monitoring katika mikoa yote
nchini Tanzania
baada ya kufanya hivyo kwa mafanikio makubwa mwaka 2009.
Akizungumza na wanahabari
muda huu makao makuu ya LHRC mkuu wa dawati la uangalizi wa changuzi na bunge
bwana KHAMIS MKINDI amesema kuwa kituo chao kimesambaza waangalizi nchi nzima
katika mikoa 25 na wilaya 165 za Tanzania bara na visiwani ambapo hadi kufikia
sasa wawakilishi wao wapo kila kona ya Tanzania kwa uangalizi wa hatua kwa
hatua ya uchaguzi huo,ambapo amesema kuwa uchangalizi huo umeanza kipindi cha
kampeni na utaendelea kipindi cha uchaguzi na baadae baada ya uchaguzi.
Wataalam mbalimbali wakiwa tayari kufanya uangalizi wa uchaguzi huo |
Aidha pamoja na wawakilishi
hao katika mikoa na sehemu mbali mbali nchini kituo hicho kimeweka timu maalum
ndani ya makao makuu ya LHRC ambapo ndio taarifa zote za uchaguzi zitafikia na
kupokelewa na wataalam mbalimbnali waliobobea katika Nyanja mbalimbali.
Amesema kuwa pia wako na
kitengo maalum cha kupokea taarifa kupitia mitandao yote ya kijamii ikiwemo
facebook ambapo account yao ni www.facebook/chaguzitanzania
pamoja na mitandao yoote ya kijamii kama twitter ambapo ni @chaguzitanzania
pamoja na namba ya simu ya 0684472896 ambayo mtu yoyote anawezakutuma taarifa
mbalimbali kuhusu matuio ya chaguzi katika maeneo yao .
Huu ndio mfumo utakao kuwa unatumika kuleta taarifa zoote za uchaguzi huo wa serikai za mitaa ambapo taarifa zote zitakazoripotiwa zitaonekana hapa |
Pamoja na hayo amesema kuwa kituo cha sheria
LHRC ni commanding center ambapo lengo lao ni kupokea taarifa za uchaguzi na
kuzifikisha katika mamlaka husika kwa lengo la kuzifwatilia
Wataalam wakiwa kazini kuhakikisha mambo yote yanakuwa sawa |
Akitaja baadhi ya taarifa
ambazo wanaendelea kuzipokea katika maeneo mbalimbali ni pamoja na
uandikishwaji wa wapiga kura kuwa wa muda mfupi na wengi kushindwa
kujiandikisha,kuenguliwa kwa wagombea kinyume cha taratibu,pamoja na matatizo
mengine ambao wamezitaka mamlaka husika kuzifanyia kazi taarifa hizo
No comments:
Post a Comment