Pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Hawa Gasia akizungumza na Waandishi wa Habari leo Picha na Suleiman Magari |
Na Karoli Vinsent
SERIKALI nchini imekili Uchaguzi uliomalizika jana wa Serikali za Mitaa ulikuwa na Dosari katika baadhi ya Maeneo mbalimbali nchini na kusema itawachukulia Hatua kali za Watendaji Halmashauri Mbalimbali waliopelekea kuwepo na Dosari hizo.
Pia Licha ya kuwa na Dosari lakini Bado Serikali imesema uchaguzi huo umefanikiwa kwa asilimia 98,Tofautisha na Miaka mingine.
Hayo yemesemwa leo Jijini Dar Es Salaam naWaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Hawa Gasia wakati wa Mkutano na Waandishi ili kuzungumzia uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa ambapo pamoja na Mambo Mengine Waziri Gasia alikili kuwepo na Dosari kwenye Vituo mbalimbali vya kupiga kura katika baadhi ya Kata,Vijiji,Mtaa au Vitongoji
Waziri Gasia alizitaja Dosari hizo ambazo ni kukosekana na Ujio wa Vifaa vya Kupigia Kura,Kasoro za karatasi za kupigia kura,wapiga kura majina yao kutokuwepo katika vituo pamoja na kuwepo na udangachifu kutoka kwa wapiga kura.
Pichani ni Waandishi wa Habari kutoka Vyombo vya Habari Tofauti wakimsikiliza kwa makini Waziri Hawa Gasia |
Vilevele Waziri Gasia alisema Halmashauri na Maeneo yenye Kasoro ambayo hayakufanya Uchaguzi,yatarudia uchaguzi huo ndani ya Siku (7) kama kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa zinavyoelekeza.
Aidha,Waziri Gasia aliitaja Mikoa ambayo Dosari zilijitokeza na kupelekea kuhailishwa kwa uchaguzi huo katika baadhi ya Kata, vitongoji na Vijiji ni, Kilimanjaro , Manyara,Morogoro,Shinyanga,Simiyu,Kigoma,Mwanza,Tabora,Tanga,Mara,Rukwa,Dar Es Salaam,pmoja na Mkoa wa Pwani.
Waziri Gasia aliongeza kuwa kwa ujumla Halmashauri ambazo hazinadosari ni 145 kati 162 zilizofanya uchaguzi ambapo Halmashauri tatu kati ya hizo hazikufanya Uchaguzi kabisa kutokana na kucheleweshwa kwa Vifaa.
Hatahivyo Waziri Gasia aliziagiza Halmashauri hizo uchaguzi kufanya haraka ndani ya siku 7 na vilevile Wizara hiyo ya TAMISEMI itawachukuli hatua kali za watendaji waliopelekea Dosari hizo.
“Tumeitaka Mikoa Iwasilishe Taarifa rasmi na kamiilifu kuhusu Kilichojitokeza katika Halmashauri hizo na Wizara itachambua taarifa hizo ili kubaini wote waliosababisha kasoro wachukuliwe hatua stahiki ikiwemo kusimamisha kazi,kukatwa mishahara,pamoja na kufukuzwa kazi”alisema Waziri Gasia.
Waziri Gasia aliongeza kuwa licha ya uchaguzi wa mwaka huu wa Serikali za Mitaa kuwepo na Changamoto mbalimbali lakini serikali imefanikiwa uchaguzi huu kwa asilimia 98 tofautisha na miaka mingine.
No comments:
Post a Comment