Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF profesa IBRAHIMU LIPUMBA akizungumza na wanahabari mapema leo makao makuu ya chama hicho Buguruni Jijini Dar es salaam |
Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF
Profesa IBRAHIM LIPUMBA amemtaka Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Rais
JAKAYA KIKWETE kuwawajibisha waziri mkuu wa Tanzania mh MIZENGO PINDA pamoja na
waziri wa tamisemi mh HAWA GHASIA kwa kushindwa kusimamia vizuri uchaguzi wa
serikali za mitaa huku akiwaita kuwa ni mizigo kwa rais na haibebeki.
Akizungumza
na wanahabari makao makuu ya chama hicho asubuhi ya leo LIPUMBA amesema kuwa
chama chake kimesikitishwa sana na mwenendo mzima wa uchaguzi huu pamoja na
zoezi nzima la upigaji kura ambapo amesema kuwa zoezi hilo liligubikwa na
sintofahamu kadha wa kadha na kusababisha vurugu katika baadhi ya vituo.
Akitaja
baadhi ya mbinu chafu ambazo amesema kuwa zilifanywa na serikali ili
kuwadhoofisha wapinzani ni pamoja na wagombea wengi wa upinzani kuenguliwa siku
moja kabla ua uchaguzi na wengine siku ya uchaguzi,uchaguzi kutokuanza kwa
wakati katika maeneo mengi ya Tanzania,uchaguzi kusogezwa mbele bila sababu ya
msingi katika wilaya nyingi,pamoja na matukio mengine mengi yakiwemo ya vurugu
na uchakachuaji ambapo amesema kuwa ni ishara tosha kua uchaguzi huu haukuwa wa
haki.
“ndugu
wanahabari lazima mh Rais atumie busara kama anataka kumaliza kipindi chake
bila mizigo ni lazima akubali kuitua mizigo ambayo inaonekana wazi kuwa
inamuelemea na wa kwanza ni waziri mkuu mizengo pinda ni mzigo ambao lazima Rais
akubali kuutua ili mambo yakae sawa”amesema lipumba.
Wanahabari wakisikiza kwa makini |
Amesema kuwa matukio
yaliyojitokeza katika uchaguzi wa seikali za mitaa mwaka huu yamedhihirisha
wazi tamko lao ambalo wamewahi kulitoa kuwa serikali wamekurupuka
kutangaza uchaguzi wa serikali za mitaa na hawajajipanga kusimamia uchaguzi
huo.
Aidha
amesema kuwa wananchi sasa wamechoka na ufisadi wa mali za umma unaondelea na wameamua kufanya mabadiliko
hivyo hivyo huku akiwataka wanachi kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha
katika daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kufanya mabadiliko hayo.
Uchaguzi
wa serikali za mitaa nchini Tanzania ulifanyika jumapili ya wiki ya jana ambapo
iliripotiwa kuwa na dosari nyingi katika maeneo mengi jambo ambalo limekuwa
likilalamikiwa na watu wengi kuwa wizara husika imeshindwa kusimamia uchaguzi
huo
No comments:
Post a Comment