Wednesday, January 28, 2015

DRFA YAWAOMBA WAPENZI WA MPIRA WA MIGUU KUJITOKEZA KWA WINGI MICHEZO YA TAIFA CUP

2
Uongozi wa chama  cha soka mkoa wa Dar es salaam,DRFA,umewaomba,mashabiki na wote wenye mapenzi mema ya kandanda,kujitokeza kwa wingi kuzishangilia timu za Dar es salaam zinazoshiriki ligi kuu,Daraja la kwanza na michuano ya taifa Cup wanawake ,ili kutoa hamasa kwa wachezaji.
Leo (januari 28) kutakuwa na mchezo mmoja wa ligi kuu kwa timu ya Simba ya Dar es salaam dhidi ya Mbeya City ya Mbeya,mchezo ambao utakaopigwa katika uwanja wa taifa jijini.
Itakumbukwa kwamba katika mechi mbili za ligi msimu uliopita,Simba na Mbeya City hakuna aliyefanikiwa kumfunga mwenzake,na kujikuta wakiambulia sare ya 1-1 kule uwanja wa Sokoine,na ule wa marudiano uliopigwa kwenye uwanja wa taifa nao kwenda sare ya 1-1.

Katika michuano ya taifa Cup,Temeke na Ilala zimefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali baada ya kupata ushindi kila moja katika mechi za robo fainali zilizopigwa leo (januari 27),ambapo Temeke imeiangamiza bila huruma Mbeya mabao 3-0,huku Ilala ikiizodoa Iringa kwa mabao 2-1.
Aidha DRFA imeipongeza timu ya Kinondoni ambayo haikufanikiwa kuingia katika hatua ya mtoano,kwa juhudi kubwa na ushindani iliouonesha licha ya kuondolewa katika hatua ya makundi.
Viongozi wa DRFA wamekuwa mfano kwa kujitokeza kushuhudia mechi hizo za Taifa Cup,Ligi kuu na zile za Daraja la kwanza,ili kuongeza chachu kwa timu za Dar es salaam kufanya vizuri.

No comments: