Kufwatia sakata la mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF profesa
Ibrahim lipumba Jana kukakamwa na kupigwa katika maandamano ya chama
chake huko temeke sakata hilo limetua bungeni asubuhi hii na kusababisha
bunge kahirishwa kutokana na wabunge wa upinzani kuwasilisha hoja ya
kuahirisha shughuli za bunge.kujadadili jambo la dharura lililojitokeza.
Akiwasilisha hoja hiyo mwenyekiti wa NCCR MAGEUZI JAMES MBATIA
ameliomba bunge kutoka na uzito wa jambo hilo na ukizingatia heshima
aliyo mayo lipumba na kitendo alichofanyiwa paMoja na kutii amri ya
polisi ni kitendo cha kihuni na hakivumilki hivyo bunge lijadili jambo
hilo.
Mheshimiwa
MBATIA amesema kuwa Lipumba ni mwenyekiti wa chama ambacho kina
wabunge zaidi ya 30 huku bungeni,lipumba ni mwenyekiti wa chama ambacho
kinashiriki serikali ya umoja wa kitaifa huko zanzibar,haiwezekani
atendendewe kitendo kama kile kilichotokea jana,naomba mwongozo wako
spika ili tusitishe mambo ya leo na tujadili jambo hili ambalo ni kubwa
na haliwezi kufumbiwa macho
.
Baada
ya kuwasilisha hoja hiyo wabunge wa upinzani walisimama ishara ya
kuunga hoja mkono hapo ndipo spika makinda alipowataka wakae na swala
hilo litapatiwa majibu na serikali hapo kesho.
Baada
ya majibu hayo wabunge wa upinzani hawakuridhika na wakaendelea
kusimama hadi spika akaamua kulisitisha bunge hadi SAA kumi Leo.
No comments:
Post a Comment