SHEKH RAJAB KATIMBA ambaye ni katibu wa shura ya maimamu nchini Tanzania akizngumza na wanahabari mapema leo nje ya mkutano huo |
Baada ya aliyekuwa waziri wa nishati na madini
nchini Tanzania profesa SOSPETER MUHONGO jana kutangaa rasmi kuachia ngazi
kutokana na tuhuma za ukwapuaji wa mabilioni kwenye account ya ESCROW wadau
mbalimbali wametoa maoni yao juu ya sakata hilo na jinsi linavyoshughulikiwa.
Mmoja kati ya watu waliozungumza na mtandao huu ni
SHEKH RAJAB KATIMBA ambaye ni katibu wa shura ya maimamu nchini Tanzania ambapo
leo wanafanya kongamano la maimamu jijini Dar es salaam kwa lengo la
kuwakumbusha waislamu wote nchini juu ya majukumu yao katika jamii kwa ujumla.
Akizungumza nje ya kongamano hilo shekh RAJAB
amesema kuwa kitendo cha mawaziri na viongozi waliohusika na ESCROW kutangaza
kujiuzulu kimya kimya bila hatua zaidi kufwatwa ni usanii mkubwa kwan sio
utatuzi wa sakata hilo na badala yake wanapumzika baada ya kufanya ufisadi huo.
Amesema kuwa njia sahihi ni kuwashuhulikia wahusika
kwa mujibu wa sheria na sio kujiuzulu pekee kwani haitoshi.
“nitolee mfano swala la jana la waziri MUHONGO
kujiuzulu na kusisitiza kuwa yupo safi kabisa,na wakati yeye hana mamlaka ya
kujisafisha ila kuna vyombo ambavyo vinaweza kusema kuwa yuko safi ni kitendo cha
kuwahadaa watanzania”amesema shekh katimba.
Maimam mbalimbali ambao wamehusdhuria katika semina hiyo |
Ameongeza kuwa hatua zinazoeendelea kuchukuliwa na
serikali pamoja na mamlaka husika juu ya sakata hilo ni za kupongezwa japo kuwa
zimechelewa sana na watu wameiba na kujulikana zamani ila wamekuwa wakiachwa kimya
kimya
Katika hatua nyingine shekh KATIMBA ameendelea kusisitiza
kuwa mchakato wa kupakana kwa katiba umejawa na usanii na utapeli mkubwa ambao
uko wazi huku akitolea mfano swala lao wanalolidai kwa muda mrefu la kupatikana
kwa makahakama ya kadhi ambalo limekuwa likipigwa kalenda kila linapoibuka
ambapo amesema kuwa wataendelea kudai hadi kieleweke.
Amesema kuwa kutokana na wao kutokusikilizwa juu ya
madai yao kwenye katiba sasa wanajipanga kuwahamasisha watanzania na waislam
wote kwa ujumla kuususia mchakato wa katiba mpya kwani hauna manufaa kwa
watanzania wote bali ni kwa watu wachache tu.
No comments:
Post a Comment