Sunday, January 25, 2015

KAULI ZA DK SLAA NA ZITTO NA MNYIKA KUHUSU WAZIRI MUHONGO ZIKO HAPA

Kufuatia hatua  ya Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Sospeter Muhongo kujiuzulu katika  nafasi  hiyo ya  uwaziri,  mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Mh Zitto Kabwe amepongeza uamuzi huo wa Prof Muhongo ambapo amesema kuwa hatua hiyo ni heshima kubwa kwa bunge.
 
"Napenda kuchukua nafasi hii kutambua busara aliyochukua ambayo naamini itasaidia harakati za kujenga demokrasia yenye uwajibikaji. 
 
"Naamini uamuzi wa Ndugu Muhongo umewezesha kulinda heshima ya Bunge na maazimio yake. Kwa muda mfupi alioongoza Wizara hiyo, Ndugu Muhongo ameweza kuongoza mabadiliko kadhaa muhimu ya kiutendaji katika wizara hiyo na taasisi zake. 
 
"Hata hivyo, nafasi ya Wizara aliyokuwa anaongoza katika suala la Tegeta Escrow imemtia doa kubwa ambalo ilikuwa lazima awajibike. 
 
"Naamini Rais Kikwete atamteua mtu mchapakazi na makini zaidi atakayeweza kuendeleza yale mazuri ya Ndugu Muhongo na kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza." Amesema Zitto kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Docta slaa akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu amejibu hivi

Dokta Slaa ameitoa kauli hiyo mda huu wakati akizungumza na Mwandishi wa mtandao huu ambaye alitaka kujua baraza hilo jipya kwa upande wao wanalizungumziaje pamoja na mambo mengine alisema Rais kikwete anataka kulizima sakata la ufisadi wa Escrow katika kuwachagua watu ambao hawana jipya.
 
“Baada ya kuaona mambo yameaanza kumwendea hovyo kwenye chama chake ameanza kulivunja baraza la mawaziri mimi naona baraza hilo halina jipya limejaa watu wezi wenye nia ya kuendelea kuliibia taifa na watanzania wasitegemee makubwa”
 
“Kwani ufasadi wa Escrow umemgusa hata yeye mwenywe kikwete kutokana na mfanyakazi wake aliyemtuma kuchukua pesa kwenye Akaunti iliyofunguliwa kwenye benki ya Exim  kwa kumtuma bwana Guromu kuchukua pesa,leo anakimbilia kulivunja baraza la mawaziri hiyo haina jipya” alisema Dokta Slaa.
KAULI  YA  JOHN  MNYIKA 
 



Mhe. John Mnyika (MB) - Baraza bado ni dhaifu , Rais alipaswa kutumia mabadiliko haya kuondoa mwaziri wote ambao walisemwa na upinzani, wananchi na hata baadhi ya wana ccm wenyewe kuwa niu mizigo. Badala yake mabadiliko haya pamoja na kuziba mapengo ya Muhongo na Tibaijuka, yamelenga kupunguza majeraha ya mivutano ya ndani kwa ndani ya baraza la mawaziri.
 
Ofisi ya waziri mkuu na ofisi ya Rais kutokana na makundi ya urais ya ndani ya ccm. Wananchi wasitegemee mabadiliko makubwa kutokana na baraza hili na yasitumike kuwapa matumaini hewa wananchi kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015 abadala yake nguvu zielekezwe kujiandikisha kupiga kura, kuiondoa ccm uchaguzi 2015 kuwezesha Braza la Mawaziri la 
 
UKAWA kuteuliwa na kuongoza mabadiliko nchini.
Aidha mabadiliko ya baraza hili hayatazuia haja ya Serikali kutoa taarifa Bungeni juu ya utekelezaji wa maazimio yote ya Bunge juu ya kashfa ya Escrow na hoja ya kutaka mchakato wa kura ya maoni usitishwe na maandalizi yaendelee kuwezesha uchaguzi ujao kuwa wa huru na haki kuwezesha mabadiliko ya kweli kwa manufaa ya nchi na wananchi.
Baraza hilo aliloliteua rais jana hili yapa
 
Mabadiliko ya Mawaziri
.Mawaziri wawili wamejiuzulu
i) Ardhi-Tibaijuka
ii)Nishati na madini-Sospeter Muhongo
Walio teuliwa
1. George Simbachawene- Waziri Nishati
2.Mary Nagu-Waziri wa Nchi mawasiliano na Uratibu
3.Christopher Chiza-Waziri uwezeshaji na Uwekezaji
4.Halson Mwakyembe-Ushirikiano wa afrika mashariki
5.Lukuvi-Ardhi Nyumba na Makazi
6.Steven Wasira-Kilimo chakula na Ushirika
7.Samwel Sitta -Wizara ya Uchukuzi
8.Jenista Muhagama-Sera na uratibu wa Bunge

No comments: