HABARI zilizotufikia mda huu zinasema Jeshi la Polisi Mkoani Dar es Salaam limetumia nguvu kwa kurusha mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchama cha Wananchi CUF waliokuwa kwenye maandamo wilaya ya Temeke .
Na kufanikiwa kuwatia nguvuni viongozi waandamizi wa chama cha Wananchi CUF,wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa Ibrahimu Lipumba,huku wananchi wa maeneo hayo wakiishi kwa hofu kubwa sana.
Akithibitisha kukamatwa viongozi hao pamoja na kuvunjwa kwa maandamano .Afisa Habari wa chama cha Cuf ,Bwana Silas alipoongea na mtandao huu amesema waalianza maandamano ya Amani katika Viwanja vya temeke na kwenda mbagala , ambapo maandamano hayo yaliokuwa na lengo la kumbukumbu ya mauaji ya wanachama wao yaliofanyika TAREHE 26 januari mwaka 2001 huko Zanzibari na Tanzania Bara,
Bwana Silas alisema wakati wapo kwenye maandamo hayo walipofika maeneo ya Mtongani iliyopo wilaya ya Temeke ndipo Jeshi la polisi likafika na kurusha mabomu na kuwapiga wanachama wa chama hicho na kufanikiwa kuwakamata viongozi wa chama hicho,na kuwapeleke kituo kikuu cha polisi.kwa madai maandamano hayo hayana ruhusa
No comments:
Post a Comment