Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu Bi HELLEN KIJO BISIMBA akizngumza na wahabari mapema leo |
Sakata la kupigwa na kudhalilishwa kwa mwenyekiti wa
chama cha wananchi CUF Profesa IBRAHIMU LIPUMBA katika maandamano ya chama
hicho juzi huko Temeke limeendelea kulaaniwa kila kona ambapo leo kituo cha
sheria na haki za Binadamu nchini Tanzania LHRC wameibuka na kauli ya kulaani
kitendo hicho na kusema ni kitendo cha kinyama na kinachoididimiza democrasia
ya Tanzania.
Akizungumza
na wanahabari katika mkutano wa wadau mbalimbali wa kujadili mapungufu ya
katiba pendekezwa na sheria ya kura ya maoni Mkurugeni mtendaji wa kituo hicho
Bi HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa vyama vya siasa vipo kwa mujibu wa sheria
na katiba ya Tanzania na maandamano ni haki ya kila mtanzania hivyo kitendo
kinachofanywa na polisi kujaribu kuwanyamazisha watanzania kwa kuzuia
maandamano ambayo ni ya amani ni kitendo kibaya na kisipopigwa marufuku
kitalipekeka taifa la Tanzania mahali ambapo sio pazuri.
Mwanasheria kutoka LHRC HAROLD SUNGUSIA akizungumza katika mkutano huo ambao unafanyika katika ukumbi wa ubungo plaza jijini DAR ES SALAAM |
Katika mdahalo huo ambao
umehudhuriwa na baadhi ya wanahaharakati wa kuitafuta katiba akiwemo aliyekuwa
mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba HAMFREY POLEPOLE na wadau
wengine wameendelea kupinga kwa kasi mchakato wa kupata katiba kuendelea kwa
kile ambacho wanadai ni kukosa uhalali wa kisiasa na mapungufu mengi ambayo
yapo katika sheria ya kura ya maoni ambayo itasimamia mchakato huo
Wadau mbalimbali wakiwa katika mkutano huo |
No comments:
Post a Comment