Meneja Mkazi wa Coca-Cola Tanzania Yebeltal Getachew
akizungumza na waandishi wa habari
katika uzinduzi wa kampeni ya Share a Coke leo jijini Dar-es-salaam.Hebu fikiria
utajisikiaje inapotokea mtu maarufu akakutambua na kukutaja jina lako katikati
ya umati mkubwa wa watu! Ni furaha iliyoje, kwani sasa Kampuni ya Coca-Cola
inatoa fursa hiyo kwa wateja wake kupitia kampeni mpya inayojulikana kama ‘Share
a Coke’.
Kampeni hiyo inatoa fursa kwa wateja wa Coca-Cola
kuweka majina ya marafiki, ndugu au familia zao kwenye sehemu ya nembo ya maarufu
ya Coca-Cola. Kampuni ya Coca-Cola imechapisha zaidi ya majina 200 ambayo ni maarufu miongoni mwa vijana wa Kitanzania.
Katika hatua
ya uzinduzi wa kampeni hiyo mpya, Kampuni ya Coca-Cola iliweza kuwafurahisha
wapenzi wake hususani vijana wenye ushawishi kutoka katika vyombo vya habari na
burudani pamoja na mashirika kwa kuwapatia kinywaji murua cha Coke huku kopo la
kinywaji hicho likionyesha majina yao ikiwa ni hatua ya kampeni hiyo ya aina
yake na ya kipekee.
Katika hafla
ya kutangaza uzinduzi wa kampeni hiyo inayosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa Coke,
waandishi wa habari, wamiliki wa blog na wenye mitandao ya kijamii, walipata
fursa ya kupata kinywaji hicho murua huku makopo ya Coke yakionyesha majina
yao, hali inayoashiria kuwa kinywaji hicho ni maalum kwao! Kwa mujibu wa
maofisa wa Kampuni ya Coca-Cola, hatua hiyo inalenga kuleta furaha ya pamoja na
wapenzi wao kwa miezi minne ijayo.
“Share a
Coke inatoa
fursa na uzoefu wa pekee kwa wateja wetu na kuwafanya wajisikie raha kwani Coke
inakuwa imetengenezwa mahsusi kwa ajili ya mteja mwenyewe ambaye kampuni
inamthamini zaidi. Kupitia kampeni hii, tutaendelea kusambaza furaha zaidi kwa
wateja wetu majumbani, katika mijumuiko ya kijamii, shuleni, vijijini na
migahawa huku tukiendelea kuwaunganisha watu pamoja,” alisema Yebeltal Getachew ambaye ni Meneja Mkazi wa Coca-Cola
Tanzania.
Licha ya
kuwa kampeni hii ya Share a Coke inawalenga zaidi vijana, inatoa pia fursa kwa
wateja wote wa Coca-Cola kuamua na kufurahi na watu muhimu katika maisha yao
kwa kunywa kinywaji wakipendacho cha Coke huku kopo likiwa na jina watakalo
kulingana na utashi wao. Miongoni mwa majina maarufu 200 yanayotumiwa na vijana
kama vile Chris badala ya Christopher
au Jerry badala ya Gerald ni kati ya
mambo yaliyo katika kampeni hii. Aidha, ipo fursa kwa wateja kuamua mengine
zaidi kadri wapendavyo.
Meneja
Masoko wa Coca-Cola Tanzania, Maurice Njowoka, anasema kuwa Kampuni hiyo
itapanua zaidi kampeni hiyo kupitia mitandao ya kijamii ili kuwawezesha wateja
kupata nafasi ya kuchagua majina wanayoyataka wakati wowote huku wakiburudika
na kinywaji hicho. Kwa wale wenye shughuli mahsusi kama vile harusi au sherehe
za kumbukumbu ya jambo fulani pia wana nafasi nzuri ya kupata kinywaji cha Coca-Cola
kikiwa ndani ya makopo yaliyoandikwa majina ya washiriki katika hafla husika.
“Coca-Cola ni
kinywaji kinacholeta burudani kwa kila mmoja. Kwa mantiki hiyo, tunahakikisha
kuwa Watanzania wanapata fursa ya kuamua juu ya nani wafurahi naye pamoja
kupitia kinywaji cha Coke popote pale walipo,” alisema.
Bidhaa za Coke
zenye majina maalumu kulingana na utashi wa mteja zinapatikana katika maduka
makubwa ya rejareja, maduka ya kawaida au vioski, hoteli na migahawa katika
maeneo yote nchi nzima. Aidha, Njowoka alisema kuwa kampeni hiyo itajumuisha
pia misemo maarufu inayotumika mitaani kama vile ‘Mshkaji’ na mingine mingi ili kupanua wigo zaidi na kutoa fursa
kwa wateja kuwa karibu zaidi na watu wawapendao.
Kampuni ya
Coca-Cola itatoa fursa hiyo kwa wateja kwa kuishirikisha mitandao ya kijamii
kama vile Facebook, Twitter au Instagram pamoja na majukwaa mengine yanayotoa
fursa za matangazo ya biashara ili kuwawezesha wateja kukata kiu yao kadri
wapendavyo. Wateja wataweza si kuagiza tu Coke yenye jina lake, bali pia mteja
ataweza kutuma picha, au video za matukio ya kukumbukwa kwenye mitandao ya
kijamii akitumia jina la kampeni kupitia: #ShareACokeTZ.
Coca-Cola ikiwa ni Kampuni ya vinywaji
baridi inayoongoza duniani, inajulikana sana kwa kuongoza soko la Tanzania kwa
kampeni na ubunifu katika masoko. Hivi karibuni imefanikiwa kuzindua kampeni
mbalimbali zilizofanikiwa sana. Miongoni mwa kampeni hizo ni pamoja na Sababu
Bilioni za Kuiamini, Upande wa Coke wa Maisha, Brrrr
na nyinginezo ambazo zilipokewa vizuri na wateja wa Tanzania.
Mwisho…/
|
No comments:
Post a Comment