Msanii wa music wa kizazi pipya diamond akizungumza na wanahabari juu ya huduma hiyo na jinsi alivyoipokea |
Kampuni ya simu ya TIGO TANZANIA leo imetangaza
uzinduzi wa muziki wa tigo ujulikanao kama TIGO MUSIC kwa kushikiana na DEEZER
ambayo ni huduma ya kimataifa inayorusha music itakayowapa watanzania music
usiokuwa na kikomo.
Mwana FA naye ni mmoja kati ya wale ambao watakuwa katika show hiyo ya uzinduzi pale LEADERS CLUB |
Akizundua huduma hii mpya
meneja wa chapa wa TIGO WILLIAM MPINGA amesema kuwa kuanzia January 24,wateja
wa tigo wenye vifurushi vya malipo ya kabla ya internent wana uwezo wa kupata
nyimbo million 36 za wasanii wa kitanzania na Africa kwa ujumla katika simu zao
za mikononi na za smartphone.
Amesema kuwa vile vile tigo
itatafuta miziki mipya ya kusisimua ya wasanii wa ndani kupitia ushirikiano
mpya wa kampuni ya Africa music rights ambayo inawezesha kutafuta na kusimamia
haki za music katika bara la Africa .
Ali Kiba atakuwepo |
Huduma hiyo itazinduliwa rasmi
mnamo January 24 mwaka huu katika viwanja vya leaders ambapo kutafanyika hafla
ya uzinduzi ambapo wananchi watapata burudani ya kutosha kutoka kwa wasanii
maarufu na mahiri kutoka Tanzania kama diamond,alikiba,profesa j,vanesa
mdee,ben paul,isha mashauz,malaika band,yamoto band,msondo,na wengine kibao
kutoka Tanzania ambapo kiingilio kitakuwa ni bure Tamasha ambalo limepewa jina la KIBOKO YAO
Weusi nao walizunguma na wanahabari juu ya jinsi walivyojiandaa na show hiyo |
Aidha amesema kuwa mabali na
kuwapa wateja nafasi ya kupata music kupitia huduma hiyo pia wasanii wa Tanzania
itakuwa ni nafasi kwao ya kujiongeea kipato kutokana na nyimbo zao ambazo
zitakuwa zimesikilizwa kupitia huduma hii ambapo tigo itawapa wasanii hao
mafunzo jinsi ya kutumia na kunufaika na huduma hii.
Meneja wa chapa wa TIGO WILLIAM MPINGA akizngumza na wanahabari juu ya huduma hiyo |
Kuanzishwa kwa huduma hiyo ya
TIGO MUSIC nchini Tanzania kumetokana na mafanikio ya uzinduzi wake nchini
Ghana mwaka 2014 na America ya kusini mwaka 2012,tangu kuanzishwa kwake imekuwa
ni sehemu muhimu kwa maisha ya kidigital ya watu ya kila siku nah ii inaendana
na matukio ya music ya ana kwa ana yaliyowahi kufanywa na wanamusic mashuhuri
duniani pamoja na yale yaliyorekodiwa ndani ya studio
PICHA ZAIDI ZIPO CHINI------------
No comments:
Post a Comment