Sunday, January 4, 2015

MBIO ZA URAIS--WAZIRI MEMBE AJIPIGIA PROMO KIAINA KANISANI LEO

Waziri wa mabo ya nje na ushirikiano wa kimataifa mh BERNARD MEMBE akizungumza na waumini wa kanisa la kianglican jjjini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya kanisa hilo

 Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa mh BERNAD MEMBE amesema kuwa yeye ni mmoja wa viongozi wa Tanzania wasiojihusisha kwa namna yoyote katia rushwa naufisadi waaona yoyote hiyo anasifa ya kuitwa kiongozi bora na kuwataka watanzania kuwapiga vita viongozi wanaotaka madaraka huku wakiwa na skendo za ufisadi katika maeneo mbalimbali nchini.

                    Waziri Membe ameyasema hayo leo jijini dares salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya kanisa la kianglican yaliyofanyika katika kanisa la mt ALBANO POSTA Jijini Dar es salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi wa sherehe hiyo,waziri membe amesema kuwa miaka 50 ya kanisa hilo ni miaka mingi na kama kanisa ni muda wa kujitafakari nakuona wapi walikosea ila kama serikali na viongozi wa kisiasa nimuda wakujitafakari nakubadili mienendo yao ili wawatumikie watanzania kwahali na mali.

 Akizungmziamwakawa 2015 na uchaguzi ujao waziri Membe amesema kuwa ni muda sasa wa Tanzania kuwapiga vita viongozi ambao wanataka madaraka kwa kupitia rushwa naufisadi nakuwachagua Viongozi waadilifu zaidi ili waweze kuwatumiakia kwauadilifu huku akigoma kujitaja kama yeye ni mmoja wa viongozi wanaofaa kuchaguliwa katika nafasi za uchaguzi ujao mwaka  huu.
waziri membe amesema kuwa yeye hapendi rushwa na hataki hata kuiskia nani lazima watanzania wote wazungumze lugha moja hiyo ili kuwasaidia watanzania kupata viongozi waadilifu katika uchaguzi ujao.

Waziri membe ambaye alionekena kushangiliwa sana na waumini wakanisa hilo aliungwa mkono na askofu mkuu wakanisa hilo askofu VALENTIN MOKIWA na kusema hiyo ndio aina ya viongozi wanaotakiwa na watanzania wanaozungumza mambo yanayowahusu watanzania .

Ikumbukwe kuwa waziri membe amekuwa akitajwa sana katika wale viongozi ambao wanautaka urais wa Tanzania na mara kadhaa harakati zake zimekuwa zikionekana waziwazi . 
Waumini wakimpigia makosi kwa wingi baada ya hotuba yake


Waziri membe alizindua rasmi safari ya miaka 50 mingine ya kanisa hilo


No comments: