Pichani ni ,Mwenyekiti wa Jumuiya ya vijana wa Chama cha Wananchi CUF-JUVICUF,Hamidu Bobali, Akizungumza na Waandishi wa Habari leo,jijini Dar es Salaam |
NAKAROLI VINSENT
JUMUIYA ya Vijana ya chama cha Wananchi CUF-JUVICUF wametangaza kuanzisha maandamano makubwa ya kulaani vitendo wanachodai ni vya ukiukwaji wa Haki za Binadamu kilichofanywa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi CCM,cha kumpiga Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa Ibrahimu Lipumba na wanachama wao, walipokuwa kwenye maandamo.
Kauli hiyo JUVICUF imekuja siku moja wakati Bunge likiwa limefunga Mjadala ulioibuliwa na Mbunge wa Kuteuliwa James Mbatia juu ya kupigwa mwenyekiti wa chama cha Wananchi CUF,Profesa Ibrahimu Lipumba,na Bunge kufikia maamuzi ya pamoja kuiachia mahakama kutoa hukumu.
Akitangaza Maandamano hayo leo Jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Jumuiya ya vijana wa Chama cha Wananchi CUF-JUVICUF,Hamidu Bobali,wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo alisema chama hicho kimepokea kwa masikitiko makubwa uongo ulitangazwa na Waziri wa Mambo ya Ndani nchi Mathias Chikawe wakati alipokuwa akitoa taarifa Bungeni.
“Tunasikitisha sana juu ya kauli iliyotolewa na waziri Chikawe ndani ya Bunge jana kwa kuweka uwongo mwingi kwenye taarifa yake kwa kumsingizia profesa wetu kwamba alikiuka sheria, sio kweli kwani profesa alikuwa sahihi,na ndio maana tunaandaa maandamano sisi Vijana wa Chama hicho ili kulaani vitendo vya kinyama na vya kuwapiga viongozi wetu na wanachama chetu”alisema Bobali.
Bobali alibainisha kuwa Jumuiya ya hiyo vijana kufuatia matukio hayo wanamtaka Rais Jakaya kikwete kuomba Radhi watanzania juu ya matukio hayo ya kupigwa na kudhalilishwa pamoja kuvuliwa kwa viongozi wetu na jeshi la polisi.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza kwa Makini |
Aidha,Jumuiya hiyo alimtaka Waziri wa mambo ya Ndani,Mathias Chikawe,pamoja Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu kujiuzulu kwenye Nafasi zao kutokana kitendo chao cha kudanganya Umma kwa kusema Maandamano hayo yalikuwa hayana kibali.
Vilevile,Mwenyekiti huyo wa Vijana alisema Tarehe ya Maandamano itatangazwa mda wowote kuanzia sasa na kuwataka wananchama hao kuwa na subira kuwaachia viongozi wa chama hicho
No comments:
Post a Comment