NA KAROLI VINSENT
SIKU moja kupita baada Mwenyekiti
wa Chama cha Wananchi CUF,Profesa Ibrahimu Lipumba kupandishwa mahakamani
kwa kile kinachodaiwa kushawishi wanachama wa chama hicho kuandamana na kupelekea jeshi hilo kutumia
nguvu katika maeneo ya Mtongani wilaya ya temeke Jijiji Dar es Salaam.
Nacho
Chama cha Wananchi CUF,kimeibuka na kulivaa jeshi la polisi nchini na kusema
jeshi hilo linatumiwa na chama cha mapinduzi CCM,ili kudhoofisha upinzani nchi.
Kauli
hiyo imetolewa Leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu mwenyekiti wa Chama cha
wananchi Cuf ,Juma Duni Haji,Wakati wa Mkutano na waandishi wa
Habari ili kuzungumzia kitendo alichofanyiwa mwenyekiti wa chama hicho cha
kupigwa na polisi,ambapo Bwana haji alisema Chama hicho kinalaani vikali kile
alichodai ni hujuma wanachofanyiwa na polisi Kuzoofisha upinzani nchini.
“Cuf-tunalaani
kitendo hicho cha jeshi la polisi nchini kutumika kisiasa kuzuia shuguli halali
za vyama vya upinzani nchini na kuwaruhusu ccm kufanya wanavyotaka bila
kubughudhiwa na vyombo vya dola wala kisingizia vya sababu za kintelijinsia”
“Kumkamata
mwenyekiti wetu wa taifa,kumdhalilisha pasipo kuwepo kwa maandamano ambayo
CUF na viongozi wake walishakubaliana kutofanya”alisema Bwana Haji.
Bwana
Haji aliongeza kuwa licha ya kulaani kupigwa kwa mwenyekiti wao pia wanalaani
kupigwa hata kupigwa wananchama wao ambao wanadai walikuwa hawana kosa lolote.
Aida,Bwana
Haji alibainisha kuwa hata hoja wanayoisema jeshi la Polisi kwamba chama hicho
kilidharau magizo ya jeshi la Polisi,kuendelea na maandamano hayo kwa kusema
sio kweli kwani chama hicho kilifuata maagizo yote.
Vilevile,Bwana
Haji alilitaka jeshi la polisi kuacha kutumika na chama cha mapinduzi
CCM kwani wanachokifanya hakikubaliki na chama hicho kitachoka na kuongeza kuwa
kuchoka huko kutapelekea Taifa kutotawalika na amani ya nchi itakuwa
imevurugika
Bungeni
Mjadala uliendelea Hivi.
Baada ya Jana Spika Anna Makinda kuliharisha
Bunge mara mbili jana ili kupisha Serikali kupeleka Taarifa kamili ya Jeshi la
Polisi kutumia nguvu ya kubwa ya Mabomu kuwapiga wananchama wa CUF,waliokuwa
wakiandamana kuadhimisha kumbukumbu ya Mauaji yanayodaiwa kufanya jshi la
Polisi huko Zanzibar Januari 26 na 27 Mwaka 2001 na kupelekea vifo vya watu
zaidi ya 30.Bunge hilo lilendelea Leo-
Kwa
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Bwana Mathiasi Chikawe akitoa Taarifa kwaniaba
ya Serikali ambapo alisema Jeshi la Polisi lilikuwa Sahihi kutumia nguvu
kuwatawanya wananchama chama cha Wananchi CUF kwa madai Jeshi hilo lilitoa
taarifa za kubaini kumekuwa kunawatu wanataka kuvuruga amani kwenye maandamno
hayo na chama hicho kikakaida taarifa hizo.
Baada
kutoa Tamko hilo kwa niaba ya Serikali na pia Waziri mwenye Dhamana Jeshi la
Polisi nchini.
Ndipo
Mwanasheria Mpya wa Serikali Gorge Masanju akamtaka Spika Anne
Makinda kuacha kulizungumzia Suala hilo kwa madai tayari lipo katika Mahakama
na kuendelea kufanya hivyo kugonganisha Mihimili miwili kati ya Bunge na
Mahakama.
Kauli
hiyo ya AG Masanju ikapingwa na Spika makinda na Kutaka Majadala uendelee.
Wabunge
wakaachangia
Wabunge walipota kuchangia wa kwanza alikuwa
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambapo yeye alikituhumu chama cha
mapinduzi CCM,kwa kulifanya jeshi la polisi kuwa watu wao na kumuomba Waziri wa
Mambo ya Ndani Chikawe ajiuzulu.
“Jeshi letu letu la polisi limetekwa nyala na
element la kifashisti,tena zinaungwa ndani ya CCM na serikali yake,kumbe
tunapigwa kutokana na hao ambao wanasema tupigwe tu,leo nashangaa waziri
chikawe na waziri mkuu kwanini wasijiulu”
“Sheria za vyama vya siasa zinasema wazi
nashangaa huyo waziri chikawe anayesema ambayo atakiwi kuwepo hapo,sheria
haziwapi mamlaka kuvuzuia maandamano’alisema Lissu.
Gwiji
huyo wa Masuala ya Sheria nchini ambaye pia ni Mwanasheria mkuu wa Chadema
aliendelea kuongea kwa uchungu akisema hakuna mbunge wa upinzania asiyepigwa
na jeshi la polisi.
“Watu
wetu wameuliwa na jeshi la polisi na mwangosi kauawa na jeshi la polisi leo RPC
Kamuanda aliyemua kupandishwa cheo,watu wetu wameuwa na jeshi la polisi,leo
nashangaa waziri huyu anakuja kudanganya bunge hivi”
“Katika hali hii lazima bunge lifikie maamuzi
la kuwajibishe hao wenye mamlaka wanao hamulu sisi kupigwa ,ambaye ni waziri
mkuu,na mwengine ni Waziri Chikawe nae pia aondoke kama tulivowaajibisha majizi
ya Escrow”alisema lissu.
Kwa
upande Mwenyekiti wa kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe alisema Vitendo
walivyofanya Jeshi la Polisi havikubariki na vinafaa kupigwa Vita.
Wabunge wa CCM
wanena.
Kwa upande wao wabunge wa Chama cha Mapinduzi
CCM,walitetea jeshi la Polisi na kusema kama mtu atakayekiuka sheria apigwe tu.
Kwa
upande wake Mbunge wa Jimbo
la Mtera Mh.
Livingstone Lusinde alisema jeshi la Polisi liko sahihi kwa kitendo walichokifanya
kwani viongozi wa CUF,walilenga kuvuruga Amani ya nchi.
Hali
ya hewa yachafuka Bungeni
Naye MBUNGE wa Donge, Sadifa Juma Khamis (CCM)
alichafua hali ya hewa Bungeni hapo baada ya kusema Mwenyekiti wa Chama
cha Wananchi CUF,Profesa Ibrahimu Lipumba ambaye amesema amepigwa na
kusema hajapigwa bali amegushwa.
“Huyo anayesema amepigwa lipumba,hivi kapigwa
Yule kagushwa,eti anasema waziri ajiuzulu mtu kagushwa angepigwa angetembea
Yule,eti anajifananisha rais kikwete na Lipumba na Rais wanafanana sio kweli
kwani CUF ni chama ni Saccos ili ile ni Saccos’alisema Mbunge Khamis Sadifa.
Spika Makinda aokoa Jahazi
na kumtaka Mbunge Sadifa afute kuli yake maana fujo zilianza kutoakea bungeni
Ndipo mbunge akatoa maneno ya Saccos.
Mjadala
ulipokwisha.
Kwa upande wake Mtoa hoja Mbunge wa Kuteuliwa
James Mbatia alikubaliana na Bunge kuacha mahakama iachiwe na kusema
serikali inatakiwa iondoe ukiritimba ulioko ndani ya jeshi la polisi kwa
kuondoa mfumo uliopo ambao unaleta mtafaruku kati ya polisi na vyama vya siasa.
Makinda anena.
Spika makinda alimaliza mjadala huo kwa
kusema kanuni ya 47,inahaja kuangaliwa kwamba jambo hilo sio la dharula bali ni
la muhimu na kusema mjadala huo uishia hapo na kuiacha mahakama kufanya kazi yake.
No comments:
Post a Comment