Balozi wa Canada Nchini Tanzania akimkabidhi tunzo Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania-TAMWA. |
Katika hali ya kutambua mchango mkubwa wa mkurugenzi
mkuu wa chama cha wanahabari wanawake Tanzania TAMWA bi VALERIE MSOKA,balozi wa
Canada nchini Tanzania ALEXANDER LEVEGUE leo amemkabidhi mkurugenzi huyo tuzo
ya umahiri na utambuzi wa jitihada zake katika kukomesha ndoa za utotoni na
vitendo vya ukeketaji nchini Tanzania.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo mkurugenzi
huyo VALERIE MSOKA pamoja na kumshukuru balozi wa CANADA kwa kutambua mchango
wake amesema kuwa bado Tanzania inapita
katika changamoto kubwa ya mwaswala ya ndoa za utotoni katika mikoa mingi kama
shinyanga,Dodoma,mara na mikoa mingine ambapo amesema kuwa nguvu kubwa sana
hasa kutoka serikalimi imahitajika katika kupigana kuokoa watoto wa kike ambao
wanakumbwa na kadhia hiyo ikiwa ni pamoja na kutekeleza sheria ambazo
zinawalinda watoto wa kike nchini.
Mkurugenzi wa TAMWA VALERIE MSOKA akizungumza na wanahabari kuhusu tukio hilo |
Awali wakati akikabidhi tuzo hiyo balozi wa Canada nchini
ALEXANDER LEVEGUE amesema kuwa licha ya Tanzania kupiga hatua katika
kukabiliana na ndoa za utotoni na maswala ya ukeketaji amesema bado maeneo
mengi jitihada kubwa zinahitajika ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa jamii juu
ya madhara ya mila hizo ambazo zimekuwa zikiwatesha hasa watoto wa kike katika
maeneo mengi nchini.
Wanahabari na wadau mbalimbali waliohudhuria katika shughulli hiyo |
Katika hafla hiyo fupi pia ilihudhuriwa na katibu
mkuu wa wizara ya maendeleo jinsia na watoto ANNA MAEMBE ambapo pamoja na kumpongeza mkurugenzi wa
TAMWA kwa tuzo aliyopata amesema kuwa jumla ya watoto 2 kati ya 5 nchini Tanzania
wameolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18 huku hatari ya vifo na kuongezeka
ugonjwa waq fistula na magonjwa ya kuambukiza yakiongezeka kwa kasi.
No comments:
Post a Comment