Mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu mapambano ya kukomesha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino),Said Ndonge akiwa na wajumbe wa kamati hiyo, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maandamano wanayotarajia kuyafanya Machi 3 Mwaka huu jijini Dar es Salaam. (Picha Emmanuel Massaka).HABARI KWA HISANI YA MICHUZI BLOG |
Kamati ya kuratibu mapambano ya kukomesha mauaji ya watu
wenye ulemavu wa ngozi (Albino)umepingana na kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa
Chama Cha Watu Wenye Ulemavu Ngozi Taifa, Bw. Ernest Kimaya kuwa kamati iliyoandaa
matembezi ya hisani ni ya watu wahuni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar, Mwenyekiti wa Kamati
hiyo, Bw, Said Ndonge amesema kauli ya mwenyekiti wa Taifa ni ya ubaguzi na inatoa
nafasi ya adui kuendelea kwa mauaji ya jamii yetu.
Amesema tangu mwaka 2006
waliouwawa ni 76 na 15 kubaki na ulemavu wa kudumu "Hivyo sisi
wanaharakati wa kupambana na kukomesha udhalimu huu tunaendelea kulaani vitendo
wanavyotutendea baadhi ya jamii yenye imani potofu za kishirikina.
Kamati hiyo imesema haiutambi umoja wa chama cha
AlbinoTanzania kutokana na viongozi wake kushindwa kusimamia majukumu yake
na badala yake kutaka kuleta mfumo wa kubaguana na kumfanya adui apate nafasi
kutushambulia.
Hata hivyo, Bw. Ndonge amesema maandamano yako palepale kutokana na Jeshi la
Polisi kutoa ulinzi kwa siku ya maandamano
yanayotarajiwa kufanyika Machi 2 mwaka huu.
Kamati hiyo imetaka wadhili wajitokeze kufadhili maandamano
hayo katika kuokoa watu wenye ulemavu wa ngozi.
No comments:
Post a Comment