Baada ya kusambaa habari mbalimbali ambazo
zilitangazwa na mmoja wa chama cha ACT Tanzania kuwa wabunge wawili wa kutoka
chama cha NCCR mageuzi amba ni FELIX MKOSAMALI na DAVID KAFULILA watakihama
chama hicho na kujiunga na ACT wabunge hao wameibuka leo na kutoa tamko kali.
Wakizugumza na wanahabari leo mapema katika ofisi za
chama chao jijini Dar es salaam wabunge hao wamesema kuwa ni kweli kuwa
wameziskia habari hizo katika magazeti mbalimbali ambazo zimesemwa na mmoja wa
viongozi wa ACT lakini hazina ukweli na hazitakaa ziwe za ukweli kwani hawana
muda wa kufanya jambo la ajabu kama hilo.
FELIX MKOSAMALI akizungumza kwa mshangao mkubwa
amesema kuwa ni habari ambazo zinachekesha kuona chama kama ACT kinatumia
majina yao kutaka kujitangaza kwani hakuna ukweli wa habari hizo.
“naomba nisema kitu kimoja naomba chama cha ACT
watafute mbinu na njia nyingine ya kukikuza chama chao na sio njia hiyo
wanayotumia kutumia majina ya wabunge kama sisi kujitangaza”alisema mkosamali
Aidha DAVID KAFULILA amesema kuwa yeye kama
mwanachama wa nccr mageuzi na ukawa haoni haja ya kuhama kwani ukawa ni
kimbilio la watanzania wengi hivyo kuhama ni sawa na kuchanganyikiwa na kukosa
dira katika siasa.
Habari mbalimbali katika vyombo vya habari leo
zilimnukuu kiongozi wa ACT kigoma akieleza kuwa wapo katika mazungumzo ya
mwisho na wabunge hao kujiunga ndani ya chama hicho kipya.
No comments:
Post a Comment