Mwanamitndo maarufu nchini Tanzania ambaye amekuwa
akifanya shughuli zake nchi za ujerumani na marekani TAUSI LIKOKOLA amerejea
nchini baada ya kukaa nje ya Tanzania kwa Zaidi ya miaka 10 ambapo ameeleza
mambo mbalimbali atakayoyafanya kipindi atakapokuwepo Tanzania.
Miss TANZANIA 2014 ndiye aliyeongoza mapokezi hayo jioni hii katika uwana wa ndege kumpokea mwanamitindo huyo mwenye makazi yake nchini marekani |
Akizungumza na mtandao wa HABARI24 BLOG uliopiga
kambi katika uwanja wa kimataifa wa mwalimu nyerere kusubiri ujio wake mrembo
huyo ameueleza mtandao huu kuwa amefurajhi sana kuwa nchini Tanzania baada ya
kipindi kirefu kuwa nje ya nchi ambapo amesema kuwa amejifunza mengi sana hasa
katika fani hii ya wanamitindo.
Akizzngumza na baadhio ya wanahabari waliojitokeza kumpokea |
TAUSI LIKOKOLA amesema kuwa fani ya uanamitindo
nchini Tanzania bado ipo chini kwani bado hakuna uwekezaji mkubwa ambao
unafanyika kuinua fani hiyo na kunachofanyika ni juhudi za mtu mmoja mmoja huku
akitolea mfano kwa wanamitindo waliofaniiwa kama FLAVIAN MATATA kuwa wametumia
juhudi binafsi kufikia hapo walipo.
Ngoma ndiyo asili ya mtanzania tucheze kidogo |
Amesema kuwa ni lazima sasa watanzania na wadau mbalimbali
kuelewa kuwa fani ya mitindo ni fani ambayo inaweza kuwasaidia vijana hivyo ni
bora ikapewa kipaumbele na kuona inawasaidia vijana katika hali na mali.
TAUSI LIKOKOLA ambaye ni mmoja kati ya wanamitindo wa
kwanza kabisa kufanikiwa kufanya kazi za mitindo kimataifa miaka ya 90 ambapo
alifanikiwa kufanya kazi na makampuni makubwa ya marekani pia ni mwandishi wa
vitabu mbalimbali amekuwa msaada mkubwa wa mawazo kwa wanamitindo wa kitanzania
ambao wanafanya vizuri sasa kama FLAVIAN MATATA,MILLEN MAGESE,HERIETH PAUL na
wengine wengi.
Mwanamitindo huyo ambaye amepokelea na aliyekuwa
miss Tanzania bi SITTI MTEMVU atakuwa nchini Tanzania kwa siku kumi ambapo
atafanya shughuli nyingi za kijamii ikiwemo kuzindua manukato yake
mapya,kusaini vitabu vyake ambapo pia atakwenda visiwani zanzibari kwa ajili ya
kufanya shughuli mbalimbali za kijamiii kabla ya kurudi nchini marekani.
Mtandao wa HABARI24 BLOG upo sambamba kukueleza kila
atakachokifanya katika ziara hiyo
PICHA ZINGINE ENDELEA CHINI |
No comments:
Post a Comment