Saturday, February 28, 2015

MAUAJI YA ALBINO NCHINI YAMGUSA MWANAMITINDO TAUSI LIKOKOLA,AUTUMIA USIKU WA JANA KUCHANGISHA FEDHA ZA KUWASAIDIA

Mwanamitindo mkongwe kutoka nchini tanzania TAUSI LIKOKOLA akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla yta chakula cha jioni iliyoandaliwa rasmi kwa ajili ya kuchangisha fedha ziweze kuwasaidia watu wenye uhitaji maalum ikiwemo watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na watu wanaoishi na virusi vya ukimwi

 Baada ya kukaa nje ya Tanzania kwa zaidi ya maika kumi na hivi majuzi kurejea kwa kipindi kifupi nchini  mwanamitindo maarufu na mkongwe TAUSI LIKOKOLA usiku wa kamkia leo ameendesha shughuli ya kuchangia fedha kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye matatizo ya ulemavu wa ngozi pamoja na waathirika wa ugonjwa wa ukimwi nchini ikiwa ni sehemu ya mwanamitindo huyo kurudisha shukrani kwa watanzania kwa kumpokea tena nchini.


Shughuli hiyo ambayo imeendeshwa jijini Dar es salaam imeshughudia watu mbalimbali kujitokeza kwa wingi kumpa saport ili kufanikisha lengo lake hilo ambalo ni jambo ambalo limepongezwa na watanzania wengi kwani kuna watu wengi wenye uhitaji na inahitajika watu kama TAUSI wengi ili kuwasaidia watanzania.
Akizungumza na mtandao huu katika hafla hiyo ya chakula cha jioni iliyokwenda sambamba na harambee hiyo mwanamitindo TAUSI LIKOKOLA amesema kuwa ni miaka mingi amekuwa nje ya Tanzania na baada ya kurejea kwake amesikitishwa sana baada ya kukuta tatizo ambalo limeanza kuwa sugu la mauaji ya watu ambao wana ulemavu wa ngozi jambo ambalo amesema kuwa limemsukuma kuanza kuwasaidia watu hao kwani kwa sasa wanaishi katika mazingira yasiyo sala sana.

Mmoja kati ya waandishi nguli  na wasomi nchini Tanzania GENERALI ULIMWENGU alikuwa ni mmoja kati wa wageni waalikwa katika shughuli nhiyo ambapo amempongeza TAUSI kwa wazo lake hilo la kuwasaidia watu wenye uhitaji kwani ni baraka hata kwa mwenyezi mungu

Amesema kuwa ni jambo la kutisha sana kuona au kusikia mambo ambayo wanakutana nayo walemavu wa ngozi nchini Tanzania na hata ukisikiliza story zao jinsi wanavyoishi bila amani lazima itakugusa ambapo amesema kuwa ni wakati sasa wa watanzania kukemea kwa lugha moja tatizo hilo ili likome na lisijirudie tena.

Alikuwepo pia,aliyekuwa miss Tanzania mwaka 2014 SITTI MTEMVU akiwa anashughudia hafla hiyo kwa ukaribu kabisa
Aidha katika hatua nyingine mwanamitindo TAUSI LIKOKOLA ameitumia hafla hiyo kuzindua manukato yake mapya pamoja na vitabu ambavyo ameviandika mwenyewe aambapo alitumia bidhaa hizo katika kupiga mnada ili kupata fedha aweze kuwasaidia watu wenye uhitaji maalum nchini tanzania.
Mbunifu wa mavazi maarufu nchini TANZANIA MUSTAFA HASANALI ambaye usiku huo ndiye aliyemvalisha TAUSI LIKOKOLA naye alikuwepo katika hafla hiyo

Tupige na sisi picha utotue kwenye blog--sawa nikawapiga
ENDELEA KUANGALIA PICHA NYINGI ZA TUKIO HILO HAPO CHINI











Mmoja kati ya walemavua ngozi nchini ambao wamekutwa na maswaibu ya kukatwa mikono yake na watu akielezea jinsi gani anamshukuru TAUSI kwa mchango wake 











Burudani ilikuwepo kama kawa


No comments: