Sunday, March 1, 2015

MCT WAANZA KUUELEWA MCHANGO WA BLOG TANZANIA

Mgeni rasmi katika Mnuso wa bloggers ambae pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga akitoa mawili matatu kwa bloggers na kuahidi kuwa kuanzia mwaka huu bloggers wataingia katika tuzo mbalimbali zinazoendeshwa na MCT 
 Mrs Jeff (kushoto) akiwa na Mrs Ankal (Katikati) na Shamim Mwasha wa 8020 fashion blog wakati wa mnuso wa bloggers
 Gadiola kutoka Wazalendo 255 Arusha(Kulia) akiwa na Ankal (Katikati) na ZAinul Mzige kutoka dewji blog
 Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga akisalimiana na Mmiliki wa Lukaza Blog, Josephat Lukaza wakati wa mnuso wa wamiliki wa Blog uliofanyika usiku wa Kuamkia Jana katika Hoteli ya Serena. Wanaoshuhudia pembeni Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN) Joachim Mushi na Mmiliki wa Michuzi Blog, Issa Michuzi
 Mgeni rasmi katika Mnuso wa Bloggers ambae pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) akijadiliana jambo na Adela Kavishe ambae ni Mmoja kati ya wamiliki wa blog hapa Tanzania, Katikati ni Monica Joseph
 Baadhi ya Bloggers wakiwa katika picha ya Pamoja
 Cheers
 Khadija Kalili akisalimiana na Mgeni rasmi ambae pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga wakati wa mnuso
 Mwenyekiti wa muda wa Mtandao wa Wamiliki wa Blog Tanzania (Tanzania Bloggers Network) Joachim Mushi akimkaribisha Mgeni rasmi kwaajili ya kutoa maneno mawili matatu kwa wamiliki wa blog.
 Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twisa akiongea jambo mbele ya Wanablog na wageni rasmi juu ya udhamini mkuu walioutoa katika mnuso huo kwa kutambua mchango wa blogs Tanzania
 Burudani kutoka kwa Jhikoman
 Mgeni rasmi akikata ndafu 
Mwakilishi wa Bloggers akilishwa ndafu na mgeni rasmi Katika Mnuso huo
 Adela Kavishe na Mdau Faustine Ruta wa Bukoba wadau Blog wakiwa mbele ya Ucanon wa Lukaza Blog
 Serebuka Serebuka unaweza pendwa tena……..
 Faustine Ruta wa bukoba wadau blog katika ucanon wa Lukaza Blog na Josephat Lukaza
 Makala na Woinde kwa pamoja
 Monica Joseph na Mkurugenzi wa Masoko Wa Vodacom Kelvin Twisa
Ankal akiwa na Faustine Ruta na Crant wakati wa mnuso wa bloggers.
Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

No comments: