Tuesday, March 31, 2015
MANENO MAZITO ALIYOYATOA GWAJIMA JANA BAADA YA KITINGA POLISI
Kuipigia kura ya Hapana Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la katiba,ambapo amesema atalipinga hata kama serikali ikimwekea vikwazo.
Kauli kiongozi wa huyo wa Kiroho ameitoa jana kwenye Makao Makuu ya Jeshi la polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ambapo alipojisalimisha ili kuhojiwa mara mwisho baada ya kutoka kwenye Hospitali ya TMJ, Mikocheni Dar es Salaam alupolazwa kutokana kuugua gafla wakati akiwa kwenye mahojiano na Jeshi la polisiwiki iliyopita.
Akiongea na waandishi wa Habari kwa kujihami mara baada ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi Wilaya kinondoni na kupewa Dhamana na kituoni hapo huku wakijazana waamani wake waliojitokeza na kumpokea Askofu wao.ambapo amesema hawezi kutishika wala kuyumbika kutokana na vikwazo anavyowekewa na Serikali juu ya kuwatetea anaodai wakristo nchini ambao wamewekewa Katiba anayoiita ni mbovu.
“Mimi nimetoka kwa amani nashukuru sana mungu animeponya salama,ila nasema sitoacha kusema ukweli juu ya wakristo wenzangu ambao anakandamizwa na mifumo ya Katiba ambayo inaonekana wazi”Amesema Askofu Gwajima.
Askofu Gwajima ameongeza kuwa kwa kuwataka viongozi wenzake kuheshimu tamko la Jukwaa la Kikristo na hata yeye mwenyewe amesema ataliheshimu sana.
TAARIFA KAMILI KUHUSU ASKARI WALIOUAWA HUKO MKURANGA PWANI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na
Polisi Mkoa wa Pwani linaendesha oparesheni kali ya aina yake ya kuwasaka watu
wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliowavamia, kuwauwa askari wawili na
kumjeruhi mmoja na kisha kupora bunduki aina ya SMG.
Tukio hilo limetokea tarehe 30/03/2015 majira ya saa mbili usiku huko
barabara ya Kilwa Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani. Katika
tukio hilo majambazi wapatao 8 hadi 10 wakiwa na mapanga na silaha zingine
waliwavamia ghafla askari watatu waliokuwa kazini katika eneo la kizuizi cha
Polisi kilichopo kijiji cha Kipara mpakani Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga
Mkoa wa Pwani. Majambazi hao wakiwashambulia ghafla askari hao kisha kupora
silaha aina ya SMG ikiwa na risasi 30 ndani ya magazine na kutokomea
kusikojulikana.
Majina ya askari wa Wilala ya Kipolisi ya Mbagala waliouawa ni kama
ifuatavyo:
1. D.2865 SGT FRANCIS,
2. E.177 CPL MICHAEL,
Askari mwingine mwenye namba D.5573 D/SGT ALLY amejeruhiwa kwa risasi
kwenye paja la mguu wa kushoto na amelazwa katika hospitali ya Temeke kwa
matibabu. Askari huyu kabla ya kujeruhiwa alipambana vikali na majambazi hayo
kwa kutumia bunduki aliyokuwa nayo aina ya SMG ambayo pia walishindwa kumpora
hivyo wakatokomea kuelekea pori la vikindu.
Katika oparesheni hiyo, nguvu na mbinu zote za kipolisi zitatumuika
ambapo vikosi vya Dar es Salaam na Pwani vilianza kufanya oparesheni hiyo mara
baada ya tukio ili kuhakikisha kwamba majambazi hao wanapatikana haraka
iwezekanavyo.
Pamoja na oparesheni hiyo kali inayoendelea, Jeshi la Polisi
linachunguza ili kubaini kama tukio hili linaashilia vitendo vya ugaidi au ni ujambazi wa kutumia silaha.
Natoa wito kwa wananchi wa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam kupitia (dhana
ya polisi jamii) kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa hali na mali kwa kutoa
taarifa sahihi.
Matukio haya ambayo yamekuwa yakitokea mkoa wa Pwani mara kwa mara ni
lazima yakomeshwe ili kuhakikisha kwamba havijirudii.
KIPAJI CHAKO AJIRA YAKO KIJANA,DC MAKONDA AJA NA HII NJEMA KWA VIJANA SASA,USIPITWE
Mkuu wa wilaya ya kinondoni DC PAUL MAKONDA akizngumza nna wanahabari mapema leo juu ya mchakato wa kusaka vipanji kinondoni ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni |
Mnamo tarehe 31 March mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amehitisha waandishi wa habari na kutangaza kuwa ameanzisha Kinondoni Talent Search ambayo itahusika kusaka vipaji vya watoto wenye vipaji kama; Kucheza, Kuimba, Kuchekesha na vingineo.
Akizungumza na waandishi wa leo alisema; ‘Kinondoni Talent Search ni mpango wenye lengo kuu la kuwatambua vijana waishio kwenye wilaya ya Kinondoni wenye vipaji vya kuimba, Kuchekesha ambao wengi wao wapo katika mazingira magumu ya kiuchumi jambo linalowafanya kushindwa kuonesha vipaji vyao mwisho ndoto zao kufifia.Hivyo, lengo kuu la mpango huu ni kuwawezesha kupata njia za kutimiza ndoto zao kupitia uwezo wao
Mwimbaji maarufu ambaye ni mmoja kti ya wanakamati wa mashindano hayo PETER MSECHU mzaa wa SOPHIA REMIX akizngumza na wanahabari leo |
Kwa ufupi ni kwamba, Kinondoni Talennt Search inalenga kwanza, kuwatengeneza nafasi za mafanikio vijana wenye vipaji, kuwapatia mafunzo na kuwaunganisha na wadau muhimu waliopo kwenye sekta zao.Lakini kubwa zaidi, kutoa hamasa kwa vijana wote wa Wilaya ya Kinondoni na Tanzania kwa ujumla juu ya umuhimu wa kuendeleza vipaji vyao, kuepuka mambo yanayoweza kuviua na kuharibu malengo yao ya baadae, mfano matumizi ya dawa ya kulevya, ngono zembe na vitendo vya uporaji.Bila kusahau kuwakumbusha vijana wote kuwa ukimiliki kipaji unakuwa ajira, ni kujua tu namna ya kukitumia ili kikufae na kukufikisha utakapo, na ndio maana kauli mbiu ya mpango huu nikipaji chako, ajira yako’ alisema.
Msanii wa vichekesho mc PILIPILI naye alikuwepo |
Ili kuhakikisha mradi huo unafanikiwa kwa kiwango cha juu na kufikia lengo, Paul Makonda ametengeneza kamati maalumu yenye wajumbe kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya pamoja na baadhi ya wasanii ambao wana uzoefu zaidi katika nyanja ambazo tunazigusa kwenye mpango huu.
1.Jumanne Mrimmy – Afisa utamaduni (Manispaa ya Kinondoni)
2.Sebastian Mhowera – Afisa Uhusiano – (Manispaa ya Kinondoni)
3.Peter Msechu – Msanii wa Bongo Fleva
4.Jokate Mwegelo – Mwimbaji/Mbunifu
5.Mc-pilipili -Mchekeshaji
MPYA--MSAADA WA HARAKA UNAHITAJIKA SINZA HAPA,TIZAMA KINACHOENDELEA
Hapa ndipo maji hayo yanapotoka ni chemba ambayo imepasuka muda mfupi uliopita lakini maji yake ni mengi kiasi kwamba yanaleta shida kubwa katika maeneo haya |
Monday, March 30, 2015
GWAJIMA MOVIE-LIPUMBA AMTEMBELEA HOSPITALINI
Profesa Ibrahim Lipumba,mchana wa Leo tarehe 30/03/2015, amemtembelea Askofu Josephat Gwajima aliyelazwa TMJ Hospital Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima aondolewa katika chumba cha uangalizi Maalum (ICU) TMJ baada ya kupata nafuu na hali yake kuendelea vizuri.
Picha za Prof Ibrahim alipomtembea Askofu Gwajima Hospitalini
TAARIFA MPYA KUHUSU WALE WALIOTAKA KUMTOROSHA GWAJIMA JANA
TAARIFA YA NYONGEZA/UFAFANUZI YA TUKIO LA KULA
NJAMA NA KUJARIBU KUMTOROSHA ASKOFU JOSEPHAT GWAJIMA AKIWA HOSPITALI
Leo tarehe 30/03/2015 waandishi wa habari walifika kituo Kikuu cha
Polisi wakitaka kujua uhalali wa silaha iliyokamatwa tarehe 29/03/2015. Silaha
hiyo ni Bastola aina ya BERRETA yenye namba CAT5802 ikiwa na risasi tatu. Pia
zilikamatwa risasi 17 za Short Gun.
Ufafanuzu ni kama ifuatavyo:
TENGA, MALINZI WAZUNGUMZIA UCHAGUZI WA CAF, FIFA
Leo Rais wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) akiwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi wamezungumzia uchaguzi wa CAF na FIFA.
Rais Tenga ameishukuru familia ya TFF kwa kumuunga mkono katika kugombea tena nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF katika uchaguzi utakaofanyika Aprili 7 mwaka huu Cairo. Tenga ni mgombea pekee wa nafasi hiyo kwa Kanda ya Afrika Mashariki na Kati.
WAZIRI LAZARO NYALANDU AHAMASISHA ELIMU KWA WATANZANIA
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGA KONGAMANO LA 3 LA VIJANA WA TANZANIA NA CHINA, JIJINI ARUSHA
Meza kuu |
KUHUSU KAFULILA NA ACT LEO,SOMA HAPA
Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, ambaye ni Katibu Mwenezi wa Chama cha NCCR-Mageuzi, amekanusha kuhamia chama cha kipya cha siasa cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania).
Kafulula amesema kuwa hana sababu ya kuhama chama hicho na kukiri kuona katika mitandao ya kujamii habari kuwa anahama chama chake na kuhamia ACT jambo ambalo halina ukweli wowote.
Amesema kuwa huenda tetesi hizo zimekuja baada ya kuwa na marafiki wengi wa chama hicho na kusema kuwa urafiki na wanachama hao hauna maana kuwa anahamia chama hicho.
Hata hivyo Kafulila amehoji ana urafiki na wanachama wa Chadema, CCM, na vyama vingine mbona hawajavitaja, na kudai kuwa Zitto, amehama kutokana na kuwa na migogoro na chama chake lakini yeye hana sababu ya kuweza kukihama chama chake.
Ameongeza kuwa atabaki kuwa Katibu Mwenezi wa NCCR-Mageuzi, na kuendelea na kampeni za kujenga chama hicho ikiwemo yeye kurudi bungeni pamoja na chama hicho kuongeza wabunge wengi zaidi.
|
Sunday, March 29, 2015
FASTJET WAZINDUA SAFARI MPYA-SASA NI KUTOKA KILIMANJARO HADI MWANZA,NA KILIMANJARO KWENDA ENTEBE UGANDA
HIVI TCRA IPO AU IMEKUFA---AMKENI MCHUKUE HATUA
“Screen shot” ikionyesha moja ya habari zilizorushwa kwenye moja ya blog uchwara kuhusiana na taarifa za uzushi wa kifo cha mchungaji Gwajima.
…Ni zile zinazoandika habari za uongo, matusi
………………………………………………………………………………………………
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Miongoni mwa mambo ambayo Tanzania tunapitia kwa sasa ni pamoja na teknolojia mbalimbali ikiwemo mawasiliano ya simu, intaneti vyombo vya habari na mengine mengi, Lakini mawasiliano hayo kwa sasa ikiwemo Intaneti wapo wanayoyatumia vibaya.
Kupitia BLOG, mtandao ambao mtu anaweza kutengeneza chombo chake cha kutolea taarifa ama kufanyaia jambo lolote lile liwafikie wengi kwa mema, lakini kwa sasa hilo halipo kwani licha ya kuwa kila mtu anaweza kuanzisha blog imetoa mwanya kwa wengine kuzitumia blog hizo kinyume na matarajio.
Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na BLOG nyingi ambazo asilimia kubwa mtu yoyote anaweza kuanzisha tena bure kama ilivyo akaunti yako ya Email, watu wanaoziendesha BLOG hizo wamekuwa wakiongoza kwa kuweka habari za uongo, upotoshaji, habari zinazoenda kinyume na maadili, pamoja na habari ambazosi za kweli.
Tunaamini wapo watu wanaofanya shughuli hizi za BLOG, ambao ni Ma-blogger wazuri tu licha ya kuwa si wanahabari, lakini kwenye blog zao wana weka ‘POST’ habari nzuri na zinazoendana na maadili pia wamekuwa wakitoa habari za kuelimisha jamii, kuifunza jamii na wanapata wasomaji wanaotembelea wengi sana kiasi cha hata kupewa matangazo na baadhi ya Makampuni binafsi ya kibiashara, Serikali na watu wengine, lakini shida ni kwenye hizi ‘Blog uchwara’ ambazo kila kukicha wao kazi yao kukopi na ku-paste habari za kwenye magazeti na kuzipa ‘kiki’ kwenye blog zao wengine habari hizo hizo za kwenye magazeti wao kazi yao kubadilisha kichwa cha ‘habari tu ilimradi apate wasomaji wengi? Jamani kweli hii ni haki?, tena kichwa hicho cha habari hakiendani na maadili ya Mtanzania ama kinakiuka maadili hii si sawa, TCRA, muamke na kuchukua hatua kali.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma.
Tunaamini Mamlaka yaa Mawasiliano Tanzania (Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), ( https://www.tcra.go.tz/) mpo na mnafuatilia lakini sijui kama mnaliona hili ni tatizo ama si tatizo.
Tukumbuke huko nyuma kulikuwa na mitandao kama hii tena ya watanzania ambao waliifungua ambapo walianza kuweka picha za kawaida na baadae ikawa inabadilika kuwa wanaweka picha za utupu… wakaachiwa hivi hivi baadae wakawa wanaweka picha za viongozi wakiwemo viongozi wakuu wa Nchi mwisho wa siku Mamlaka husika wakaja kukumbuka shuka wakati mambo yamekua si mambo.
Hivyo ni wakati sasa kwa TCRA, kuchukua hatua blog zote zinazoendana kinyume na maadili ikiwemo kupotosha, kuweka pichaa za ngono na kugombanisha watu basi zichukuliwe hatua.
Mtandao huu unaamini kuwa na unaungana na wadau wote wanaendelea kutoa maoni yao juu ya kuzitaka blog hizi zichukuliwe hatua. Kwani mpaka tunaandika habari hii ni pamoja na baada ya Mdau Yusuph Mhoja kuchukizwa na moja ya habari kwenye miongoni mwa blog hapa nchini. (Tazama picha), ambapo Mdau huyo aliuliza: “Hivi huyu mwandishi anajua kiswahili kweli? Yuko mochwari kwani amefariki huyo?” wakati anajiuliza hayo, hii ni kuwa inawatokea watu wengi sana wanaapokutana na habari kwenye hizo blog uchwara.
Wadau waliochangia mada ya Mhoja: Pendi Mahundi yeye alieleza hivi: “hahaha…. hili ndiyo tatizo kubwa la kila mtu mwenye kisimu cha TECNO bongo kujifanya blogger and a self-appointed journalist… UJINGA mtupu, huwa naziona habari kwenye viblogu mpaka kichefu chefu… full of attention-seeking sensationalism… utakuta heading: HATARI, Vilio na majonzi, Breaking news, Unbelievable..kisa tu kutaka watu wazisome blog zao.” Alieleza Mahundi.
Hata hivyo wachangiaji wengine waliomba serikali kupitisha mswada wa habari na sheria ya ICT ili kukomesha wandishi wa viblog uchwara.
Modewji blog tunaamini pia Mtandao wa wanabloga Tanzania (Tanzania Blogger Network-TBN) wapo kwani kuna misemo mingi ya zamani inayosemwa, ikiwemo ule wa SAMAKI MMOJA AKIOZA…? Jibu watatupatiaa TBN ama kama si lao basi bomu likilipuka tusimtafute mchawi huko mbeleni.
Hata hivyo, mtandao huu wa Mo dewji blog tunaungana na TCRA na kusema kuwa: “ #Ukipata ujumbe wa chuki, matusi au uongo, FUTA DELETE KABISA!.
Tuandikie maoni yako kupitia kwenye mtandao huu hapo chini ama kupitia simu 0719076376 au 0714940992
Subscribe to:
Posts (Atom)