Tuesday, March 10, 2015

BENKI YA NBC YASAIDIA WAATHIRIKA WA MVUA YA MAWE KAHAMA

Meneja wa Benki ya NBC Martin Nkanda (katikati), akikabidhi misaada mbalimbali ya kibinadamu kwa ajili ya  waathirika wa mvua ya mawe kwa wakurugenzi wa halmashauri tatu za Wilaya ya Kahama katika hafla iliyofanyika Kahama, Shinyanga juzi. Zaidi ya watu 40 walisemekana kupoteza maisha huku wengine 82 wakiachwa na majeraha makubwa baada ya mvua kubwa iliyoambata na upepo mkali kwa muda wa takriban masaa matatu kuvipiga vijiji vitatu vya Wilaya ya Kahama Machi 3 mwaka huu na kuharibu nyumba, mashamba na mifugo.  

 Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya (kulia) akimkaribisha Meneja wa Benki  ya NBC Tawi la Kahama Martin Nkanda kwenye kambi ya waathirika wa mvua ya mawe iliyopo katika Shule ya Msingi Mwakata siku Benki hiyo ilipotoa misaada.


Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Kahama,  Martin Nkanda (wa tatu kushoto)akizungumza na baadhi ya  waathirika wa mvua ya mawe( hawapo pichani) siku ya benki hiyo ilipotoa misaada. Kulia kwake ni  wakurugenzi wawili wa Halmashari za Ushetu na Msalala; Patrick Kalangwa, na Isabela Chilumba huku kushoto kwakeni  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Felix Kimario.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Patrick Kalangwa (wa tatu kushoto) akitoa neno la shukurani kwa uongozi wa Benki ya NBC kwa kutoa misaada ya waathirika wa mvua ya mawe

Meneja wa Benki ya NBC Martin Nkanda (wa nne kulia) pamoja na baadhi ya wafanyazi wenzake wakikabidhi misaada mbalimbali ya kibinadamu kwa baadhi ya  waathirika wa mvua ya mawe katika hafla iliyofanyika Kahama, Shinyanga juzi. Zaidi ya watu 40 walisemekana kupoteza maisha huku wengine 82 wakiachwa na majeraha makubwa baada ya mvua kubwa iliyoambata na upepo mkali kwa muda wa takriban masaa matatu kuvipiga vijiji vitatu vya Wilaya ya Kahama Machi 3 mwaka huu na kuharibu nyumba, mashamba na mifugo.

No comments: