Tuesday, March 10, 2015

SIKILIZA TUNDU LISU MUDA HUU AKIJIBU KWANINI WAMEMFUKUZA ZITTO HARAKA HARAKA LEO

Mwanasheria wa Chama cha Chadema Tundu Lissu leo ametangaza rasmi kumvua uanachama Mbunge wa Kigoma Kaskazini baada ya uamuzi wa mahakama juu ya kesi iliyokua imefunguliwa na Zitto Kabwe kuhusu kupinga uanachama wake kujadiliwa.
Baada ya uamuzi huo millardayo.com pia imeongea na Tundu Lissu kupata uhakika wa kinachosemekana na hizi ni sentensi zake>>’Tumemshinda,kesi yake imefutiliwa mbali amemabiwa atulipe gharama na kwa vile ile kamali aliyocheza ya kupeleka kesi mahakamani imeshindikana si mwanachama wetu tena sasa hii ni rasmi’
Sentensi nyingine Tundu Lissu amesema>>’Katiba yetu inasema ukipeleka kesi kwenye mambo ya Chama kwenye mahakama unafukuzwa uanachama na kwa mujibu wa katiba si mwanachama wetu tena,hilo haliwezi kuwa kosa letu akamuulize jaji Mchome’.SIKILIZA SAUTI YAKE HAPA CHINI KWA MSAADA WA MILAD AYYO,COM

No comments: