Thursday, March 12, 2015

DK SLAA ATINGA POLISI LEO KUMSHTAKI MLINZI WAKE

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa leo ametoka katika ofisi za Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam alipokwenda kupeleka malalamiko yake ya kutaka kuuawa na mlinzi wake aitwaye Khalid Kangezi.
Dk. Slaa amekabidhi malalamiko yake hayo kwa maandishi ambapo zaidi ya kurasa tisa amezikabidhi kituoni hapo.
Akiongea na wanahabari, Dk. Slaa amesema kuwa hajaitwa na mtu yeyote kituoni hapo kuhojiwa kama ilivyodhaniwa hapo awali bali ameenda mwenyewe kwa ajili ya kukabidhi malalamiko yake.
Dk. Slaa amekaa ofisini hapo kwa zaidi ya saa tano ambapo waandishi wa habari walizuiliwa kuingia ndani hivyo kulazimika kusubiri nje ya ofisi hiyo hadi alipomaliza kuandika malalamiko yake.SOURCE http://mzazitz.blogspot.com/

No comments: