KLABU ya Soka ya Yanga imekanusha taarifa zilizozagaa mitaani na kwenye Mitandao ya Kijamii kwamba klabu hiyo imewafukuza wachezaji wake wawili ambao ni Danny Mrwanda na kiungo wake Haruna Niyonzima kutokana na timu hiyo kupoteza mechi yake na Simba iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akikanusha taarifa hizo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari ,Mkuu wa kitengo cha Habari wa Klabu wa Yanga Jerry Murro ambapo amesema klabu hiyo haijamsimamisha mchezaji wake wala kumuita na kumuhojai kutoka na mechi ya simba.
“ Sisi viongozi baada ya mechi ya simba atukuzungumza na wachezaji wetu yeyote kabisa,tena ni mapema sana kuzungumzia hali hiyo kwani hilo ni suala ni la benchi ya ufundi na hakuna kitu kama hicho cha kufukuzwa mchezaji“amesema Murro
Murro ameongeza kuwa kwa hao wachezaji ambao wanadaiwa kwamba wamefukuzwa akimtaja Danny Mrwanda amesema mchezaji huyo anaumwa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa Maralia na Daktari wa timu hiyo amethibitisha ugonjwa wake na pia mchezaji huyo amepata kadi nyekundu kwenye mechi iliyopita ya Kimataifa.
Aidha,Afisa habari huyo akawataka wanachama na mashabiki wa Yanga kupuuza taarifa zinazoenezwa zenye nia mbovu ya kupotosha umma.
Katika hatua nyingine Klabu hiyo yenye maskani yake Jangwani jijini Dar es Salaam imetangaza rasmi kiingilio kati ya mechi yake ya kombe la shirikisho barani afrika na timu ya Fc Plantim inayotarajiwa kuchezwa mwishoni mwa wiki hii ambapo kwa mujibu wa jerry murro
Amesema Tiketi za mchezo huo zitauzwa siku ya jumamosi na tiketi zitakuwa katika mafungu mawili ambapo ni tiketi za elfu tano na elfu thelasini.CHANZO FULLHABARI BLOG
No comments:
Post a Comment