HIVI NDIVYO SIKU YA WANAWAKE ILIVYOADHIMISHWA HUKO BUGURUNI LEO.
Ikiwa leo dunia imeungana kwa pamoja kusherehekea
siku ya mwanamke duniani mpango wa taifa wa damu salama umeamua kuadhimisha
siku hiyo kwa kiuwakumbuka wagonjwa mbalimbali wa Tanzania kwa kuendesha zoezi
maalumu la uchangiaji wa damu kwa hiari ambapo zoezi hilo zimepongezwa na idadi
kubwa ya watu.
Zoezi hilo limeendeshwa katika maeneo ya bunguruni
ambapo wakazi wa mitaa hiyo pamoja nna wale waliokuwa wanapita njuia kwa moyo
mmoja wameonyesha kuguswa na matatizo ya damu kwa wagonjwa wa Tanzania na
kujitokeza kwa wingi katika uchangiaji wa damu katika zoezi hilo.
Zoezi hilo ambalo lilidhaminiwa na kampuni ya MELTD
lilifanyika katika eneo la buguruni chama ambapo mamia ya wakazi wa maeneo hayo
na viunga vyake walionekana kujitoia kwa moyo kuchangia damu ukizingatia kuwa Tanzania
bado ina upungufu mkiubwa wa damu mahospitalini.
Katika pitapita za msaka habari katika maeneo ya Dar es salaam nilifanikiwa kukutana na tukio hilo na kufanikiwa kuzungumza na baadhi
ya waratibu wa zoezi hilo kutoka mpango wa taifa wa damu salama ambapo mmoja
kati ya watu niliozungumza nao alijitambulisha kwa jina moja la bi FATMA ambaye
aliuambia mtandao huu kuwa wameamua kufanya zoezi hili hasa leo siku ya
wanawake dunian I ili kuwahamasisha watanzania kuwachangia wagonjwa walioko
mahospitalini ambao wengi pia wamo wanawake wenya upungufu wa damu .
Amesema kuwa wakazi wa maeneo hayo wamejitokeza kwa
wingi na kutia moyo kuwa mafanikio ya kupata damu ya kuwasaidia wagonjwa yapo
pamoja na changamoto yingi walizo nazo katika zoezi hilo.
Msaka habari alipozungumza na baadhi ya watanzania
waliojitokeza katika zoezi hilo wameonyesha kuvutiwa na zoezi hilo huku
wakuwasihi watanzania wengine kujitokeza katika mazoezi kama haya kwani
matatizo ya upungufu wa damu humkumba kiila mtu kwa wakati wowote hivyo ni
vyema kuwa na moyo wa kujitoa wakati ukiwa na uwezo ili pindi unapopata
matatizo uwe na wa kukusaidia.
ENDELEA KUTIZAMA BAADHI YA PICHA KATIKA ZOEZI HILO
No comments:
Post a Comment