Sunday, March 8, 2015

VIJANA WA NCCR WAWAMTOSA MBATIA,WATANGAZA WANAYETAKA AGOMBEE URAIS UKAWA


Huyo ndiye dk GEORGE LEORNAD KAHANGWA ambaye vijana wa nccr wanamtaka agombee uraisi kupitia umoja wa katiba ukawa


Katika hali ambayo haijazoeleka katika siasa za Tanzania vijana wa chama cha NCCR mageuzi leo wameibuka na kumtaja mtu ambaye wanadhani anafaa kugombea uraisi kupitia umoja wa katiba ya wananchi ukawa huku wakimpiga chini mwenyekiti wao JAMES MBATIA na kumtaja dk GEORGE LEORNAD KAHANGWA kuwa ndiye wanadhani anafaa.

Wakizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam mwenyekiti wa vijana hao wa NCCR mageuzi DEO MECK amesema kuwa dk KAHANGWA amekuwa ni mwanachama wa chama hicho mzalendo wa mkuda mrefu na msomi wa kiwango cha juu sana na mwenye vipaji vingi pamoja na sifa zote za kubeba bendera ya chama hichio katika kuelekea mbio za uraisi wa Tanzania.
Mwenyekiti wa kitengo cha vijana wa NCCR-mageuzi akizungumza na wanahabari mapema leo kuhusu uamuzi wao huo
Amesema kuwa kutokana na sifa alizonazo kiopngozi huyo wao kama viongozi wa vijana wa chama hicho kwa niaba ya vijana wote wa NCCR wanapendekeza jina hilo lipitishwe katika mchakato wa chama hicho ili kulipeleka mezani mwa UKAWA kujaribu kama litapata nafasi ya kugombea uraisi kupitia umoja huo.

Aidha amesema kuwa licha ya kumwomba dk KAHANGWA akubaliane nao pia wameahidi kumchukulia form ya kiuomba nafasi hiyo,ikiwa ni pamoja na kulipa ada ya kiuchukua form ya kugombea na pia wameahidi kupigana hadi mwisho ili wahakikishe jina hilo linapita mbele ya kamati kuu ya chama na hatimaye kupata rishaa hiyo.

 Akifafanua kwanini hawakumpendekeza kiongozi wao ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho mh JAMES MBATIA vijana hao wamesema kuwa mh MBATIA ni kiongozi shupavu na mwenye hoja nyingi ila kwa sasa anafaa zaidi kuendelea na ubunge alionao na ikizungatia kuwa amekwisha tangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la vunjo.

vyama vinavyounda umoja wa katiba UKAWA vipo katika michakato ya ndani ya vyama kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali kwa ajili ya kuisimamisha bendera ya UKAWA katika uchaguzi wa mwaka huu

No comments: