Mdau wangu nimekuwekea mkusanyiko wa video kadhaa ambazo zinawaonyesha viongozi kadhaa ambao wameshatangaza nia ya kuutaka uraisi wa Tanzania,chukua tatu hizo nyingine zitakuja tu .Video ya kwanza ni mbunge wa nzega KHAMIS KIGWANGALA akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam miezi kadhaa iliyopita ambapo ambapo alitangaza nia rasmi kuanza safari ya kutafuta nafasi ya kugombea urais kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM.
Waziri mkuu wa Tanzania mh MIZENGO PINDA akiifanya mahojiano na kituo cha televisioni cha BBC aliamua kuonyesha nia yake kuwa ana mpango wa kuigombea uraisi wa tanzania
Safari ya matumaini ilipoanza,waziri mkuu mstaafu ambaye ni mbunge wa jimbo la monduli naye ni mmoja kati ya watu ambao wametangaza nia ya kugombea uraisi wa tanzania japo yeye bado anatumia misamiati migumu na bado hajawa wazi ila wachambuzi wa mambo wanasema kuwa safari ndio imeanza hiyo.
No comments:
Post a Comment