Saturday, March 14, 2015

KATIBU MKUU CHADEMA ATOA MSAADA WA BATI 850 KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO KAHAMA



Siku moja baada ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.jakya Mrisho Kikwete kushangazwa na utendaji kazi wa kamati ya maafa ya mkoa wa shinyanga  kwa kushindwa kuwahudumia waathirika wa mafuriko kwa wakati katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Mh.Dr.Wilbrod Silaa amepeleka msaada wa bati zenye thamani ya shilingi milioni kumi na mbili  akiunga mkono juhudi za serikali kwa kujali maisha ya wananchi wake.


Akizungumza  baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya waathirika wa mafuriko katika kijiji cha mwakana na kujionea hali ya uhalibifu wa mazao na nyumba kubomoka katibu mkuu chadema Mh.Dr.Willibrod Silaa amekabidhi msaada wa bati 850 na kusema kwamba watanzania wanawajibu wa kuunganisha nguvu kwa pamoja kusaidiana wakati wa majanga yanayohatalisha masiha ya watu.

Wakati huohuo halmashauri ya wilaya ya  nyang’hwale imekuwa ya kwanza kutekeleza agizo la rais kwa kupeleka msaada kwa wathirika wa mafuliko katika kijiji cha mwakata wakifatiwa na kampuni ya simu tanzania TTCL  mkoa wa shinyanga.

Akiwashukuru wahisani kwa kusaidia misaada ya chakula na bati mkuu wa wilya ya kahama Bw.Benson Mpesya amesema kuwa serikli imewajengea nyumba za muda waathirika 250 kwenye maeneo yao kwa lengo la kuondoa kambi kwenye eneo la shule ili wanafunzi waanze masomo juma tatu ijayo.

No comments: