Kwa mara nyingine tena, Mshambuliaji wa Simba Raia wa Uganda, Emanuel Okwi, amefanikiwa kuibuka Shujaa wa mchezo baada ya kupeleka furaha kwa mashabiki wa klabu hiyo akiiandikia timu yake bao pekee la ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Licha ya kubanwa mbavu na Mtibwa kwa dakika 90, Okwi alifanikiwa kuiandikia timu yake bao hilo kunako dakika 90+2 baada ya kupiga mpira kwa ustadi mkubwa kwa kuunyanyua na kumuacha mlinda lango wa Mtibwa, Said Mohhamed akiwa hana cha kufanya.
Bao ambalo Okwi amefunga leo halitofautiani sana na mabao ambayo aliwafunga Yanga pamoja na Azam FC, akimtazama kipa na kuunyanyua mpira kwa ufundi mkubwa.
Kwa matokeo hayo sasa Simba inakuwa imefikisha Pointi 29 katika nafasi ya tatu wakiwa nyuma ya Yanga wanaoongoza kwa alama 31 na Azam FC wenye alama 30 huku wakimuacha Mtibwa Sugar akibakia na pointi zake 23.
Katika mchezo huo ambao kipindi cha mwisho Simba walibadirika na kuanza kushambulia kwa kasi huku zikiwa zimebakia taklibani dakika 10 mpira uishe, Dakika ya 47 Kocha Koponovic alimpumzisha Simon Sserunkuma na nafasi yake kuchukuliwa na Ramadhani Singano ‘Messi’
Kocha Mecky Maxime aliamua kumpumzisha Ame Ally katika dakika ya 65 na nafasi yake kuchyukuliwa na Mohhamed Mpoki.
Simba walikosa bao la wazi katika dakika ya 69 baada ya mshambuliaji wake Elias Maguli kushindwa kumalizia kazi nzuri ya Emanuel Okwi ambaye aliwakokota mabeki wa Mtibwa na kuingia ndani ya 18 ya Mtibwa lakini umaliziaji ukawa duni kwa Maguli.
Dakika ya 74 Vicent Barnabas wa Mtibwa Sugar aliingia kuchukua nafasi ya Mussa Hassan Mgosi, hiyo yote ni katika harakati za kusaka pointi tatu muhimu.
No comments:
Post a Comment